Ghana:
Huduma za Mikopo kwa Wafanyabiashara katika Sekta Isiyo Rasmi
Mtandao
wa Action Reseach wa taasisi
za kukopesha mitaji midogo nchini Ghana huyakutanisha pamoja mashirika
ambayo yanajihusisha na utoaji mitaji/mikopo ya mitaji kwa wananchi
maskini wa Ghana. Kwa msaada wa Benki ya Dunia, mtandao huu ulifanya
utafiti ambao, ulitoa maelezo mafupi juu ya ubunifu usio rasmi,
ulio rasmi kidogo na rasmi kabisa (uliofanywa na taasisi za kukopesha
mitaji midogo) ambao umeanzishwa katika utoaji wa mikopo kwa wafanyabiashara
wanawake wa Ghana. Utafiti huo pia unatoa mapendekezo ya kuboresha
na kuimarisha utoaji wa huduma hiyo. Utaratibu
wa Utoaji wa Huduma za Mikopo inayowalenga Wanawake ·
Kupata
ujuzi na utaalamu wa kuweza kujiajiri. ·
Kuwa na
fursa ya kupata taarifa juu ya huduma za kimisaada za kuboresha
biashara zao. ·
Kupata
mapato na hivyo kuweza kukuza mitaji yao. Kwa
ajili ya vikwazo hivi, wanawake wengi wa vijijini wamekuwa wakijihusisha
na shughuli za ulimaji wa mazao ya chakula na shughuli zinazowapatia
kipato kidogo; wakati wanawake maskini waishio mijini wanaendesha
biashara ndogo ndogo katika sekta isiyo rasmi. Shughuli hizi zimesaidia
kidogo na wakati mwingine hazijasaidia kabisa. Hii ni kwa sababu
shughuli zenyewe za kibiashara zinakua kidogo au hazikui kabisa
na hivyo kufanya wanawake wengi kuwa kwenye kundi la maskini na
wengi wao kupatiwa mikopo na taasisi za kukopesha mitaji midogo.
Baadhi ya taasisi hizi zinalenga kuwahudumia wanawake kwa sababu
imethibitika kuwa njia hii ni ya moja kwa moja ya kupunguza umaskini
na kuongeza ustawi wa familia kwa ujumla. Katika
programu za taasisi za ukopeshaji mitaji midogo ambazo zinalenga
wanawake na wanaume, mitaji inayotolewa kwenye biashara zinazoendeshwa
na wanawake ni midogo ukilinganishwa na ile inayotolewa kwa wanaume.
Katika maeneo ya vijijini, taasisi chache za fedha zinawakopesha
wanawake wafanyabiashara. Isipokuwa pale taasisi inapokuwa na sera
mahususi ya kutenga fungu kubwa la mkopo kwa wanawake, kiasi cha
mikopo kinachotolewa kwa wanaume bado kitaendelea kuwa kikubwa ikilinganishwa
na kile kinachotolewa kwa wanawake. Lakini na hata hivyo, mara nyingi wanawake wamekuwa
warudishaji wazuri wa mikopo kwa kiwango kikubwa kuliko wanaume. Wakopeshaji
wa mikopo kwa wanawake aghalabu ni vikundi visivyo rasmi kama vile
wakusanyaji wa fedha wa kikundi cha Susu na ROSCAS; na wakopeshaji
wasio rasmi sana kama vile mashirika yasiyo ya kiserikali na vikundi
vya kijamii (CBOs). Wakopeshaji rasmi ni Benki za Akiba na Mikopo,
Benki za Vijijini na Jamuiya na vyama vya ukopeshaji. Pamoja na
taasisi hizi , programu za sekta ya umma zimeanzisha huduma za mikopo
na zinginezo kwa ajili ya walengwa. Uhamasishaji
wa uwekaji wa akiba na utoaji wa mikopo ndio huduma za kimsingi
zinazotakiwa kufanywa na taasisi hizi mbalimbali. Riba inayopatikana
kwenye akaunti za akiba ni asilimia 25 – 35 kwa mwaka. Kiwango cha
riba za mikopo kinaanzia asilimia 20 (kwa mikopo yenye ruzuku) na
kufikia asilimia 50 (kiwango cha kibiashara). Huduma zisizo za kifedha kama vile uto aji
mafunzo ya uendelezaji na ukuzaji wa biashara, ukuzaji wa ujuzi
na stadi za kibiashara na huduma za ustawi wa jamii kama vile uzazi
wa mpango hutolewa na baadhi ya taasisi za kukopesha mitaji midogo
midogo. Taasisi hizi zina lengo la kujenga uwezo wa wafanyabiashara
wadogo wadogo na kuwaendeleza kwa kuboresha utumiaji na ulipaji
wa mikopo na ustawi wa maskini kwa ujumla. Udhaifu
wa programu zilizopo Mbinu za vijijini na zile za mjini Taasisi
za fedha zinazotoa mitaji midogo midogo zinazolenga wanawake wa
vijijini, zinatumia mbinu za kukopesha wanawake waliopo katika vikundi
ili kuhakikisha uwajibika wa pamoja katika kutumia vizuri mikopo.
Mbinu hii imeonekana kuwa ya manufaa na hivyo kuongeza idadi ya
wateja wanaohudumiwa na mpango huu. Hii imeonekana ni muhimu katika
kupunguza gharama ya kufikia jamii za vijijini zilizojitenga. Mafunzo
ya uundaji vikundi pia yanawapa wanawake wa vijijini ujuzi wa uongozi
na wa kufanya maamuzi. Wanachagua
wajumbe wa kuunda vikundi, wanafanya maamuzi yahusuyo mikopo na
vilevile wanashiriki katika uendeshaji wa ndani wa taasisi zinazotoa
mitaji midogo. Taasisi
za kukopesha mitaji midogo zilizopo mijini zinalenga katika utoaji
mikopo kwa mtu mmoja mmoja kwa vile jamiia za mjini haziishi kwa
ukaribu sana kama zile za vijijini. Wateja wa taasisi hizi za mijini
kwa kawaida huenda wao wenyewe kwenye taasisi husika kwa huduma
za mikopo. Lakini katika maeneo ya vijijini taasisi hizi huwa zinawafuata
wanavijiji walipo na hivyo kufanya taasisi za mijini kuwa na gharama
ndogo za uendeshaji wa shughuli za kibenki. Taasisi
za kukopesha mitaji za Kaskazini na Kusini mwa Ghana Aina
zote za taasisi za utoaji mikopo, yaani
zisizo rasmi, zilizo rasmi kidogo, zilizo rasmi kabisa na
programu za sekta ya umma zinapatikana Kaskazini na Kusini mwa Ghana.
Taasisi za watu binafsi, kama vile benki za akaunti za akiba na
za kutoa mikopo zhupatikana zaidi Kusini mwa Ghana. Hii inatokana
na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu na shughuli za kiuchumi ambazo
zinawahakikishia wenye mabenki uendeshaji wa mabenki kwa gharama
ndogo. Kaskazini mwa Ghana kuna programu nyingi za sekta ya umma
zinazopata ruzuku kutoka serikalini. Ubunifu uliofanyika Mahusiano
ya Wakusanya fedha wa Susu na mabenki katika utoaji mikopo
Wakusanyaji
fedha wa kikundi cha Susu wanaendesha shughuli zao katika maeneo
ya vijijini na mijini ya Ghana kama mawakala wanaojitegemea. Kwa
desturi, waendeshaji wa Susu huwa ni wanaume.
Lakini hata hivyo, wanawake wachache wamejiunga na taalamu hii,
ingawaje hakuna taarifa yoyote kuhusiana na idadi yao au uwiano
wao na wanaume. Chama cha Ushirika cha Wakusanyaji wa Susu, kijulikanacho
kama GCSCA, kilichoanzishwa mwaka 1990, kimekuwa kikijaribu kuhamasisha, kuratibu na
kudhibiti shughuli za uendeshaji wa Wakusanyaji wa Susu ambao wakati
mwingine shughuli zao zimeonekana kuwa za udanganyifu. GCSCA imebainisha
malengo ya Wakusanyi hao kama ifuatavyo: ·
Kutoa
huduma ya ukusanyaji wa fedha za akaunti ya akiba kutoka kwa mtu
mmoja mmoja na kwenye vikundi vya maeneo ya vijijini na mijini. ·
Kutoa
huduma sahihi za kibenki kwa kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo
wadogo na sekta zisizo rasmi, ambao hawawezi kuacha shughuli zao
za kibiashara na kufanya safari ili kuweza kukutana na wafanyabiashara
wengine waliopo katika sekta isiyo rasmi. ·
Kuwajengea
tabia ya uwekaji akiba maskini wa vijijini na mijini. ·
Kutoa
nafasi ya kuiunganisha sekta rasmi inayoojihusisha na shughuli za
kibenki na wafanyabiashara wadogo; na ·
Kutoa
nafasi kwa watu kuweza kujiajiri wenyewe kama wakusanyaji wa fedha
wa Susu. Utaratibu
wa kawaida wa kuhamasisha uwekaji wa akiba kutoka kwa wateja ni
ule wa watumishi wa kikundi cha Susu kukusanya malipo kidogo kidogo
yanayotakiwa kukusanywa kwa mpangilio wa kila siku ama kila juma.
Mwishoni mwa mzunguko, yaani baada ya siku thelathini (30), kiasi
cha fedha kilichokusanywa kinalipwa kwa mteja ukitoa kiwango kinachokusanywa
kwa siku moja ambacho hubakia kwa wakusanyaji wa Susu kama malipo
au faida yao. Katika jaribio la kutoa huduma inayowalenga wateja,
karibu wakusanyaji wote wa Susu wameanza kuhamasisha ukusanyaji
wa fedha kuanzia mchana kila siku. Ukusanyaji wa aina hii unawapa
wateja nafasi ya kufanya biashara na kupata kiasi cha fedha kabla
ya kuweka akiba. Mbinu hii imeonekana kuwa muafaka kwa wanawake
maskini wa mijini na vijini ambao kipato chao ni kidogo sana kuweza
kuweka kiasi kikubwa cha fedha kwenye taasisi za fedha zilizo rasmi. Masoko
ndio maeneo yenye shughuli za biashara hasa zile zinazoendeshwa
na wanawake. Masoko haya yanatoa nafasi nzuri ya wakusanyaji wa
Susu kufanya kutoa huduma zao kwa gharama ndogo. Kiasi cha fedha
kinachopatikana kwa siku kinawekwa kwenye sefu majumbani au huwekwa
kwenye benki za biashara zilizo karibu kwa mtindo ule ule wa kuweka
kila siku. Wakusanyaji
wa Susu wakati mwingine huwa wanawakopesha wateja wao wenye tabia ya kuweka pesa kila siku ili waweze
kulipa ada za shule, gharama za matibabu n.k. BENKI
YA VIJIJINI YA NSOATREMAN (NRB). Katika mpango wa majaribio uliofanywa
na Benki hii, Benki iliwakopesha kwa masharti nafuu baadhi ya wakusanyaji wa fedha wa Susu ambapo nao baadaye waliwakopesha
wateja wao na kupata malipo ya kazi hii kutoka Benki hii. Benki
ya Vijijini ya Nsoatreman imekubaliana na wakusanyi hao juu ya kiwango
cha malipo wanayopata kutokana na riba inayopatikana kutoka kwenye
fedha zinazowekwa kwenye akaunti za akiba. Katika jaribio la awali
lililofanyika mwaka 1997, Benki ilitenga kiasi cha dola za kimarekani
732 kwa kila mkusanyi wa Susu aliyechaguliwa. BENKI
YA MAENDELEO YA KILIMO (ADB). Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa kutumia
tawi lake la Sunyani la Mkoa wa Brong Ahafo imeanzisha mpango wa
utoaji wa huduma za kifedha kwa kushirikiana na Tata Susu Maalum.
Fedha zinazopatikana baada ya uhamasishaji uliofanywa na Tata Susu
Maalum hupelekwa benki ambako kitengo maalum kimetengwa kuwahudumia
wakusanyaji wakati wa muda wa kawaida shughuli za kibenki. Kwa sasa
hivi kuna mpango wa kupanua utaratibu huu kwa miji mingi zaidi ya
vijiji vilivyopo karibu na Sunyani. BENKI YA AKIBA NA MIKOPO YA CITI. Benki hii imeanzisha mradi wa majaribio wa utoaji wa mikopo kwa kushirikiana na Tawi la Greater Accra la GCSCA. Katika mradi huu, wakusanyaji fedha wa Susu wenye akaunti kwenye tawi lolote la Benki ya Akiba na Mikopo ya Citi wanaweza kupewa mikopo ya muda mfupi. Mikopo hii hutolewa kwa lengo la kuwawezesha wakusanyaji watoe malipo ya awali kwa wateja wao kama watayahitaji. ACTION AID GHANA. Utaratibu ulioanzishwa na Action Aid Ghana kwa kushirikiana na Wakusanyi
wa Susu huko Kaskazini ya Ghana umetoa fursa ya kuinganisha sekta
ya huduma za kifedha isiyo rasmi na jamii za vijijini. Katika utaratibu
huu jamii zinazoshiriki katika programu ya mkopo ya Action
Aid za Bawku, Cheriponi na Tamale zinachagua wakusanyaji kutoka
katika kikundi cha Susu. Wakusanyaji hawa hutoa huduma za kukusanya
akiba na mikopo majumbani kwa wateja na mikopo iliyolipwa hupelekwa
kwenye Action Aid. MASHIRIKA
YASIYO YA KISERIKALI UHURU
KUTOKA KWENYE NJAA (FREEDOM FROM HUNGER – FFH). Freedom From Hunger
ni shirika lisilo la kiserikali la kimataifa ambalo linashirikiana
na taasisi sita za Ghana za kukopesha mitaji midogo midogo ambazo
zina programu za kutoa mikopo yenye lengo la kupunguza umaskini
na inayowalenga wanawake. Vigezo vinavyotumika kuchagua taasisi
za kukopesha mitaji midogo midogo za kushirikiana na shirika hili
ni: ·
Taasisi
lazima iwe na uwezo mkubwa wa kiuongozi na
usimamizi unaohitajika katika kuendesha programu. ·
Taasisi
lazima iwe na utaratibu mzuri wa kufikisha huduma zake kwa wanawake
walengwa. ·
Taasisi
lazima ikubali kutoa watumishi wake kwa ajili ya mafunzo ya uendeshaji
wa mikopo yanayotolewa na Shirika la Freedom From Hunger. Taasisi
sita zinazofanya kazi kwa kushirikiana na Freedom From Hunger ni Benki
ya Vijijini ya Lower Pra – iliyopo Mkoa wa Magharibi Benki
ya Vijijini ya Brakwa – iliyopo Mkoa wa Kati Benki
ya Vijijini ya Nsoatreman – iliyopo Mkoa wa Brong Ahafo. Benki
ya Wanawake ya Dunia/Ghana – iliyopo mkoa wa Greater Accra Benki
ya Jamii ya Builsa – iliyoko mkoa wa Mashariki ya Juu. Malengo
ya Programu Malengo
ya programu ya Freedom From Hunger ni ·
Kutoa
mikopo kuwepo kwa wanawake walio maskini. ·
Kutoa
elimu ya afya na lishe. ·
Kutoa
elimu ya uzazi wa mpango na kutoa taarifa. ·
Kujenga
uwezo wa taasisi za kizawa zinazotoa mitaji midogo midogo kwa kuzingatia
mafunzo na msaada wa kiufundi. Wateja Walengwa. Programu za Freedom From Hunger zinatekelezwa kwa
kushirikiana na taasisi zinazotoa mitaji midogo midogo zinazowalenga
wanawake tu kwa sababu zifuatazo: (i) matukio ya umaskini yameonekana
zaidi kwa wanawake, (ii) kuongezeka kwa kipato cha wanawake kubadilisha
hali ya maisha ya familia, na (iii) shughuli zinazoingiza kipato
zikifanywa na wanawake huhitaji mtaji mdogo. Mbinu za kiutendaji:Freedom From Hunger inatoa mafunzo kwa waendeshaji
wa mikopo walioteuliwa kutoka kwenye taasisi zinazotoa mikopo midogo
midogo katika nyanja za uanzishaji wa biashara ndogo ndogo; kutoa
elimu ya afya na lishe, uzazi wa mipango; usimamizi wa fedha; upagaji
wa bajeti na uandaaji wa mipango. Viwango vya utendaji na taasisi za
fedha za Ghana Kwa
kawaida ni taasisi rasmi za mikopo zinazozingatia viwango vya utendaji
kama vile uwiano wa mitaji. Nyingi ya taasisi zinazotoa mitaji midogo
midogo zisizo rasmi au zilizo nusu rasmi hazijaanzisha viwango vya
utendaji. Hata hivyo idadi kubwa ya taasisi hizi tayari zimeshatambua
umuhimu wa kuzingatia viwango vya utendaji ili kuhakikisha zinakuwa
endelevu. Kuhusu tathmini ya athari, baadhi ya taasisi zinazotoa
mitaji midogo midogo hufanya tathmini kila baada ya kipindi fulani
ili kuona athari ya shughuli zao kwa wateja wao. Changamoto
kwa taasisi zinazotoa mitaji midogo midogo Taasisi
zinazotoa mitaji midogo midogo nchini Ghana zinakabiliwa na changamoto
kadhaa katika utoaji wa huduma za kifedha unaofaa zaidi kwa watu
masikini, hasa wanawake. Changamoto hizi zinahusu masuala ya uchumi
mkubwa (uchumi makro), maendeleo ya kitaasisi, na njia za kuzifikia
fedha za mikopo. Lakini changamoto nyingine muhimu ni ile ya kuboresha
mbinu za kuwafikishia huduma wafanyabiashara masikini wanawake. *Kwa
maelezo zaidi juu ya mada hii tafadhali wasiliaa na: Shimwaayi Muntemba,
chumba namba j3 – 101, world bank, 1818 H Street NW, Washington
D.C. 20433. Tel. No: (202) 458-7370; e-mail address: smuntemba@worldbank.org
|