Click
one of these for: français
| português | wolof
| English
Malengo
Webu
ya Programu ya Maarifa ya Asili (MA) ni njia ya kufikia vyanzo
mbalimbali juu ya MA. Lengo lake ni kutoa fursa ya mabadilishano
ya mawazo baina ya jumuiya za wenyeji, mashirika yasiyo ya
kiserikali (NGOs), serikali, wafadhili na vyama vya kiraia. Lengo
la webu ni kusaidia kuyaelekeza maarifa ya asili katika shughuli
za washiriki wenzi wa maendeleo na kuongeza upeo wa faida
zinazotokana na misaada ya maendeleo, hasa kwa watu masikini.
Mikakati
Malengo
haya yanatekelezwa kwa kupitia mikakati mbalimbali. Mikakati hii
inajumuisha databesi juu ya maarifa ya asili na matumizi yake,
kukiwemo na chunguzi kifani zaidi ya 100 na mfululizo wa Taarifa
za MA ambazo zinatoa kwa kina utatuzi wa masuala tata mbalimbali
unaopendekezwa na wenyeji. Aidha programu inasaidia vituo vya
rasilimali barani Afrika (kwa sasa vipo vituo vinane)
vinavyojishughulisha na ubainishaji na usambazaji wa maarifa ya
asili pamoja na matumizi yake. Kwa kufanya kazi na serikali na
washiriki wenzi wenyeji, programu imeanza pia kusaidia kuelekeza
matumizi ya MA katika miradi ya Benki ya Dunia na katika programu
za maendeleo ya kitaifa .