|
Taarifa ya Majitihadi ya Maarifa ya Asili James Wolfensohn, Rais wa Benki ya Dunia, anashua Webu ya kwanza kwa Kiswahili ya Benki ya Dunia. 15 Machi, 2001 (picha) Webu hii inazalishwa na Sehemu ya Afrika na inahusika Mambo ya Maarifa ya Asili. Baadhi ya viingiziamali ni “Makala ya MA” (IK Notes) kumi na nane yaliyotafsiriwa na utangulizi wa wazo la Maarifa ya Asili barani Afrika. Maelezo mengine kutoka kwa webu ya Kiingereza yatatafsiriwa haba na haba kwa Kiswahili na lugha nyingine. Webu ya kwanza ya Benki kuonekana kwa lugha ya kiafrika, ambayo ni ya Kiwolof, ilifunguliwa na Bwana Wolfensohn mwezi wa nne, mwaka 2000. FAO (Shirika la Chakula na Kilimo): Semina ya Kimataifa ya Kwanza kuhusu Idhaa za Kilimo kwenye Redio – Februari 2001 “Teknolojia za Kutangaza na Kuwasiliana Kuhudumia Redio za Kilimo: Vipengee Vipya, Mashirika Mapya”, iliyotokea Makao Makuu ya FAO, mji wa Roma, nchini Uitalia, kutoka 19 Februari mpaka 22 Februari, 2001.
Nigeria: Serikali inatakabali matibabu ya asili kama dawa la UKIMWI – Gazeti Guardian la Nigeria, 6 Dicemba, 2000. Tarehe 5, mwezi dicemba, 2000, Waziri wa Afya Dokta Tim Menakaya alitamka kwamba, “Baada ya kuhusuriwa kwa muda mrefu kuwa chini ya uganga wa hospitali, kuanzia sasa uganga wa kienyeji na waganga wa kienyeji watapewa cheo rasmi kwenye mfumo wa afya taifani.” Mkutano Kimataifa wa Sita wa UNESCO-ACEID kuhusu ElimuTeknolojia za Matangazo kwenye Mageuzo ya Elimu kwa Maendeleo: Kuungana Maarifa Duniani na Maarifa ya Asili – 12-15 Dicemba, mwaka 2000, Imperial Queens Hotel, mji wa Bangkok, nchini Thailand. Huduma ya Usimamizi Ushirikishi wa Kuungana (PMNS) ni mradi wa pamoja wa IUCN, Afisi ya Maafikiano ya Maeneo Manyevunyevu (Ramsar) na WWF. PMNS itaunganika usimamizi kijijini, usimamizi wa pamoja, na usimamizi wa watu wa kimwetu. CGIAR – ICRAF wanatandua orodha na maelezo ya maandishi sabini na nne kuhusu majaribio na ukadirifu shirikishi ya kilimo mseto. Orodha hii inaongeza orodha ya mwaka uliopita na yamo maandishi mapya kumi na tano. Nakala za makala ya CGIAR zinapatikana kwa karatasi kutoka kwa Mercy Mwangi, lakini inabidi uagize mwenyewe vitabu na kadhalika vilivyochapishwa na taasisi za CG nyingine. Maandishi kuhusu majaribio na ukadirifu shirikishi ya kilimo mseto (Faili ya PDF KB 51) Shirika la Haki za Uvumbuzi Duniani (WIPO) inatangaza kwamba ripoti isiyomalizika kuhusu “Mahitaji na Matarajio ya Wenye Uvumbuzi wa Asili – Ripoti ya Safari za Kuchunguza Hakika kuhusu Uvumbuzi na Maarifa ya Asili (1998-1999)” sasa inapatikana kwa kutoa maoni kwenye Webu ya WIPO. Databesi ya Maarifa ya Asili ya Benki ya Dunia, na majitahidi ya WIPO kwa kumotisha jumuiya ya kimwetu kujiandikisha mifumo ya asili yao, zinaelekea hapo mbele. Mei 2000 Mkutano Kiulaya wa Nne kuhusu Madawa ya Kienyeji, 11-13 Mei, mji wa Metz, nchini France. Aprili 2000 Ramsa ya Ujuzi – Mikutano wa Msimu
Machi 2000 Mkutano wa Pili wa Maarifa Duniani, nchini Malaysia
|