|
USITAWISHAJI
WA CHAMA CHA KILIMO NCHINI MALI: Mwanzoni mwa miaka ya 1980,wanachama wa vyama vya vijijini
(associations villageoises,
au kwa kifupi AV) wa Koutiala huko Kusini mwa Mali
walikuwa na suala la kutatua na Kampuni ya Nguo ya Mali (Campagnie
Malienne des Textiles, CMDT). Uvumi ulikuwa ukienea kwamba
CMDT ilikuwa imepanga kuwaongezea malipo wafanyakazi wake
wa ugani (yaani mgao wao wa faida kutokana na pamba), bila
kuongeza bei waliyolipwa wakulima. Wawakilishi wa vyama mbalimbali
vya vijijini tayari walikuwa wameunganisha nguvu zao mwaka
1989 kutaka sera iliyochukuliwa na CMDT kuhusu wajibu wa kifedha
wa vyama vya wazalishaji ibatilishwe, matakwa ambayo hatimaye
yalikubaliwa. Wakiwa wametiwa
nguvu na ushindi huo wa awali, wawakilishi hawa waliunganisha
tena nguvu zao kukabili tatizo la bei na wakaanzisha Kamati
ya Uratibu ya Vyama vya Vijijini na “Tons” ya Koutiala, iliyojumuisha
wawakilishi wa vyama mbalimbali vya wenyeji. Wajumbe wa Kamati
ya Uratibu walijumuisha wakulima waliofuzu kisomo chenye manufaa
na wenye uzoefu katika harakati za kupigania masoko zilizokuwa
zikiendelea kusini mwa Mali tangu miaka ya 1970, na pia wawakilishi wachache wa kizazi kipya
kilichojitokeza katika muongo uliotangulia: wahitimu wa elimu
ya sekondari na vyuo waliokuwa wamerejea kwenye jumuiya zao
za asili ili kuanzisha mashamba yao. Kubadili
mfumo wa kiutawala na kisiasa Mfululizo wa mikutano na vikao ulikiwezesha kikundi kuandaa
orodha rasmi ya madai na malalamiko. Wakati huohuo, matukio
ya kisiasa yaliyoikumba Mali yalichochea mageuzi makubwa katika
vyama vya vijijini, yakipunguza zaidi faida ya mauzo ya pamba
na kuilazimisha Kamati ya Uratibu kuchukua hatua. Mnamo mwaka
1991, kikundi kiliamua kumwagiza mjumbe wake msomi kuliko
wote, mhitimu wa chuo cha kilimo aliyekuwa amerejea kwenye
jumuiya kujiunga na kilimo, azungumze na wanachama wa vyama
vya vijijini, awatulize wasiwasi wao na kuwasilisha madai
yao kwa CMDT. Jambo hili, lililolengwa kwa AV, lilifanikiwa
sana: wawakilishi wa vyama waliiunga mkono kabisa Kamati ya
Uratibu. Lakini uongozi wa CMDT, ukiwa na wasiwasi kutokana
na hali geugeu ya kisiasa, ulikataa kufanya mapatano yoyote
na Kamati hii ya wakulima. Kutokana na hali hii, kamati iliitisha
mgomo wa wazalishaji wa pamba, na wanachama wake wakatembelea
eneo lote kushawishi AV kuunga mkono mgomo. Kwa miezi miwili,
vyama viligoma kupeleka pamba kwenye CMDT, hadi Waziri wa
Maendeleo ya Vijijini alipokuja mwenyewe Koutiala kusuluhisha
mgogoro huu. Matokeo ya mapatano haya yalikuwa kwamba CMDT
ilikubali msingi wa majadiliano ya pamoja juu ya bei ya zao
kupitia shirika lisilo la kiserikali lililowakilisha wazalishaji
wa pamba. Aidha CMDT ilikubali shirika hilo kushiriki pia
kwenye Bodi ya Taifa ya kupanga bei za mazao ya kilimo. Kwa njia hii, SYCOV (Syndicate des Productears du
Coton et du Vivrier au Umoja wa Wazalishaji wa Pamba na Mazao
ya Chakula) ilianzishwa, ingawa ilichukua mwaka mmoja zaidi
kuanzishwa rasmi kisheria, kutokana na taratibu za kiutawala
zilizohitajika kutekelezwa. Uongozi wa Umoja huu mara moja
ulifungua milango ili vyama vya vijijini vya Kusini mwa Mali
vijiunge na hata ukaamua kuondoa, kwa maridhiano, ugombea
wa kiongozi mkuu wa harakati za mwaka 1991, kwa uraisi wa
Umoja huu mpya, ili kumwezesha mwakilishi wa mojawapo ya mikoa
iliyojiunga kwenye Umoja huu agombee nafasi hiyo. Umoja huu,
unaoendesha shughuli zake kwa lugha mbili (Kibambara na Kifaransa),
umeendelea kukua, bila kujali baadhi ya vipingamizi vya CMDT
na matatizo ya ndani ya Umoja yanayosababishwa na mabadiliko
geugeu ya AV, baadhi ya maamuzi tenge ya uongozi na mifarakano
kati ya uongozi wa angazi za chini (za vijijini) na wa ngazi
za juu. Kwa sasa ni sehemu ya mfumo wa kiutalawa na kisiasa
nchini Mali kwamba wakulima wana haki ya kushiriki katika
maamuzi yote ynayowahusu. SYCOV pia inandaa mafunzo ya Kifaransa
cha kuzungumza na kuandika kwa wawakilishi wa AV wanaofahamu
Kibambara tu na tayari inatumia lugha mbili (Kibambara na
Kifaransa) katika hati zake zote na katika mikutano yake. Mizizi
ya mabadiliko: kuhamishia nguvu za kiuchumi kwa wenyeji Kusema kweli, pamoja na nguvu na udhaifu ya SYCOV,
majaribio ya Umoja huu tayari
yanawakilisha hatua ya pili ya uwezeshaji wa wenyeji
katika vijiji vya Kusini mwa Mali na unaonyesha baadhi ya
faida zinazoweza kupatikana kutokana na kuhamishia mamlaka ya kiuchumi mikononi
mwa vyama vya wakulima. Ingawa pamba imekuwa ikilimwa na kuuzwa
katika maeneo haya kwa zaidi ya miaka thelathini, hali imebadilika
katika kipindi cha miaka kumi na mitano iliyopita, kutoka
ile hali ambapo wafanyakazi wa makampuni makubwa kama vile
CMDT na washirika wao walidhibiti ununuaji wa mazao vijijini
na kuyasafirisha hadi viwandani na kwenda kwenye mfumo ambapo
takribani shughuli zote hizi sasa hutekelezwa na mashirika
ya vijijini. Wawakilishi wa vyama hivi vya wenyeji au mashirikisho
ya sasa wanashughulikia kikamilifu upimaji wa uzito wa mazao,
kuwalipa wakulima, kuhifadhi mazao, kuyasafirisha hadi kwenye
viwanda vya usindikaji, na kuyauza tena kwa walaji
na kadhalika kushughulikia mipango na mahesabu na uundaji
wa sera za mashirikisho husika. Jambo hili kubwa lilifanikiwa
kwa kiwango kikubwa kutokana na programu za kisomo chenye
manufaa na elimu isiyo rasmi zilizotekelezwa kwa msaada wa
makampuni yenyewe ya pamba (au pengine programu zilizorithiwa
toka juhudi za awali za serikali ama za NGO), iliowezesha
vijana na watu wazima wenye elimu ndogo kupata stadi za kusoma,
kuandika na za kiuhasibu katika lugha zao na kuielewa vema
mifumo ya usimamizi katika lugha ya kuzaliwa ama katika lugha
mbili (ya kuzaliwa na ya Kifaransa). Hatutakuwa tunatia chumvi tukisema kuwa juhudi hizi
zimeyawezesha makampuni ya pamba kuokoa mabilioni ya faranga
(CFA francs, kwa wastani CFA 500=US$ 1). Sehemu ya kutosha
ya mapato haya imerejeshwa kwenye vyama vya jumuiya ambavyo
navyo vimewagawia wakulima kupitia vipunguo vya bei na kuchangia
kwenye mifuko ya pamoja ya uwekezaji. Kwa upande wake, mifuko
ya uwekezaji imehamasisha mfululizo wa uwekezaji mwingine
kama vile uanzishwaji wa vyama vya kuweka na kukopa fedha,
ununuzi wa zana bora zaidi za kilimo, uchimbaji wa visima
vipya vya maji, ujenzi wa kliniki na shule za jumuiya, n.k.
Hali hii ya udhibiti wa wenyeji ina uhusiano na ongezeko kubwa
la uzalishaji wa pamba katika Afrika Kusini mwa jangwa la
Sahara kwenye muongo uliopita, jambo ambalo limelipandisha
Bara hadi nafasi ya nne kwenye soko la dunia na kuzisheheneza
bajeti za kitaifa zilizobanwa sana na masharti ya programu
za kurekebisha uchumi wa nchi hizo. Pamba haiwezi kufikiriwa sana kama kichocheo cha maendeleo
endelevu, zikizingatiwa athari zake mbaya kwa rutuba ya udongo,
hasa kutokana na mfumo wa mbadilisho mazao na wa hifadhi ya
udongo unaotumika huko Afrika Magharibi. Hata hivyo, uzoefu
wa pamba umeonyesha, kwa kiwango kikubwa, uwezo wa wazalishaji
wa ngazi ya vijijini wa kuendesha wenyewe shughuli za kibiashara
na kiusimamizi – mradi wawe wamepatiwa mafunzo yanayohitajika.
Pia uzoefu huo imepelekea kuanzishwa asasi imara za vijijini
zinzotoa “mifano halisi” ya maendeleo katika nyanja kadhaa
nyinginezo. Muktadha
unaofaa: Mwingiliano wa changamoto ya kiuchumi na mtaji wa
kijamii. Vyama vya vijijini kwa kweli viliibuka kutokana na athari za mambo mawili, moja la “kimapokeo”
na jingine la kisasa; na muungano wa mambo haya mawili ndiyo
sababu kuu ya matokeo yaliyopo. Kwa kawaida jumuiya za Mali
ya Kusini zimeunganika katika “ton” (kwa lugha ya Kibambara-Kimalinke)
au miungano ya namna hii miongoni mwa vikundi vya makabila
mengine ya jirani. Vikundi hivi vya marika aghalabu husukwa
vizuri sana na vina uongozi imara. Vikundi vya “ton” ndivyo
vilivyoshughulikia masuala ya uuzaji na uwekezaji wakati CMDT
ilipofanya jaribio lake; na dhima zao mpya ziliwezesha vikundi
kubadili mielekeo yake na kuanzisha mifumo ya uwajibikaji
na mafunzo iliyokuwa bora zaidi ya ile iliyotekelezwa na vikundi
vya jando vya kimapokeo. Hivyo, kwa maana hii kushindwa, kufaulu na juhudi
anzilishi za SYCOV zinawakilisha “safu ya pili” katika kampeni
ya kukuza uwezo wa wenyeji na uwezeshaji wa vyama vya vijijini
ulioanza kwa urekebishaji upya wa mfumo wa mauzo ya pamba
miaka kadhaa iliyopita, na unaondeshwa na miundo iliyopo ya
kijamii. Na wakati huohuo juhudi hizi zimesaidia kuendeleza
mambo mengineyo. Kupeleka
maendeleo ya wenyeji kwenye safu ya pili
Mfumo mwingine mzuri: ili kuboresha usimamizi wake, vyama
vya vijijini vya kusini mwa Mali, vikisaidiana na CMDT na
msaada toka nje ya nchi, vilianzisha mnamo mwaka 1993 chombo
maalum chenye dhamana ya kukagua mahesabu yao na kutoa msaada
wa kiufundi kwa viongozi wenyeji kuhusu masuala ya kifedha. Chombo hiki kiliitwa “Kituo cha
Usimamizi cha Koutiala” (Koutiala Management Center); na tayari
kimeshaanzisha matawi yake kadha tangu wakati huo. Kituo kina
wafanyakazi kutoka vyama vya vijijini, ambao hutoa huduma
ya ukaguzi wa mahesabu kwa AV. Wafanyakazi wenyeji
hupatiwa mafunzo na kisha kusaidiwa kiufundi na wataalam
wa nje ya maeneo yao kwa muda kabla hawajajitegemea wenyewe.
Sera ya Kituo husimamiwa na Baraza la Uongozi, ambalo kwa
upande wake limeunganishwa na Shirikisho la Vyama vya Vijijini
vya Mali ya Kusini. Kinadharia, Kituo kinapaswa kuendeshwa
kwa bajeti inayolipwa kutokana na mapato ya huduma za Kituo
kwa vyama vya vijijini. Hivyo Kituo kiko katika hatua ya kati:
baina ya kuwa “kampuni tanzu kamili” ya shirikisho na shirika
binafsi la ukaguzi wa mahesabu. Lakini kwa kweli, Kituo kilianzishwa, na kingali kwa
kiwango fulani, kikitegemea msaada wa fedha toka nje. Hata
hivyo Kituo kinaonekana kumudu awamu ya kwanza ya uanzishwaji
wa uendeshwaji na
kwa hakika kinatoa huduma zinazohitajika pamoja na kuzalisha
mapato. Msingi wa makala hii ni data zilizokusanywa na Peter
Easton, Gay Belloncle, Cheibane Coulibaly, Simon Fass, Laouali
Malam Moussa na timu tano za utafiti za kitaifa wakati wa
Utafiti wa Elimu wa PADLOS kuhusu “Ugatuaji wa Madaraka na
Ujenzi wa Uwezo wa W enyej
ikatika Afrika Magharibi uliofadhiliwa na Club du Sahe/OECD
na CILSS. Kwa ripoti kamili ya utafiti wasiliana na Peter
Easton, Center for Policy Studies in Education, 312 STB, College
of Education, Florida State University, Tallahassee, FL 32306,
USA; simu (850) 644-1595;e-mail: easton@coe.fsu.edu
|