|
BURKINA
FASO: "KISOMO CHA WATU WADOGO" Nomgana ni kitovu cha shughuli cha muungano wa vijiji vya Wilaya ya Loumbila, kilichopo kilometa 30 mashariki mwa Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso. Chama cha wenyeji kiitacho Manegbzanga ("Maendeleo kwa Wote" katika lugha ya Kimoore) kilianzishwa eneoni zaidi ya muongo mmoja uliopita kwa juhudi za pamoja za wahamaji waliorejea toka nchi ya jirani ya C'ote d'Ivoire na mwenyeji mmoja aliyekuwa amekwenda kufanya kazi na shirika moja la Kiswidi lisilo la kiserikali (NGO), Organisme Suisse d'Entraide Ourriere (OSEO). Katika miaka ya hivi karibuni, chama kimeanzisha programu ya majaribio kikitumia kisomo cha Kimoore kama msingi wa kujifunza Kifaransa. Kisomo hili kimejengeka kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita na hatimaye kimekuwa mkakati mbadala wa elimu ya msingi. Kutoka kisomo cha watu wazima na kuwa mfumo mbadala wa elimu. Hata hivyo juhudi zilianza na watu wazima. Chama cha Manegbzanga kilikabiliwa mapema na tatizo la kuwapatia wanachama wake ‑ wengi wao wakiwa na elimu ndogo ama wakiwa hawana elimu kabisa ‑ nyenzo za kuwawezesha kumudu mambo yao na kushughulikia ugavi wa pembejeo za kilimo na kuwasiliana na wateja wa mazao yao walio jirani na Ouagadougou. Mtu mmoja kutoka kwenye jumuiya, ambaye awali alikuwa mtumishi wa serikali na kisha kuwa mkurugenzi wa ugani wa NGO ya Kiswidi, alianza kufanya kazi na wanakijiji kunako mwaka 1988 kuanzisha mfumo wa mafunzo ambao ungewezesha watu wazima waliosoma kwenye vituo vya kisomo kujiendeleza kwa kutumia ufahamu wa kuandika Kimoore katika kujifunza Kifaransa cha mazungumzo na maandiko. Mpango huu ulipata mafanikio makubwa na hivyo baada ya muda mfupi ukawavutia vijana wengi ‑ watoto na walio balehe ‑ ambao walikuwa wamekosa elimu ya msingi ama wamelazimika kukatisha elimu hiyo. Kamati ya kisomo ya kijiji hatimaye iliamua kukubali changamoto la kuanzisha programu ya "kisomo cha watu wadogo" (alphabetisation des tout petits). Mkakati wa mafunzo uliandaliwa kwa msaada wa wanaisimu (wataalam wa lugha) kutoka Chuo Kikuu cha Ouagadougou. Unaanzia mafunzo ya stadi za kusoma, kuandika na hesabu kwa lugha ya Kimoore na kuendelea na kujifunza Kifaransa na elimu yote ya msingi.
unaweza kutusaidia kufikiria upya namna ya kuushughulikia uwingi wa lugha wetu, jambo ambalo haliwezi kukwepeka katika mazingira yetu halisi ya Afrika. Kufupishwa kwa mzunguko wa elimu ya msingi kutatoa muda wa kupata weledi na kutumia lugha ya taifa iliyo katika maandishi kwenye mtaala wa shule . . . ..Lugha zetu zimekuwa zikidhalilishwa pasipokuwa na msingi wowote wa kisayansi kutokana to na mtazamo potofu wa wakoloni, kwani upinzani unaodaiwa kuwepo kati ya lugha za Kiafrika na lugha ya Kifaransa hauna maana yoyote. Msingi wa makala hii ni utafiti uliofanywa na watafiti kutoka Burkina Faso, Kongo na Marekani kwa msaada na ushauri wa kiufundi wa Prof Peter Easton wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Florida, wakishirikiana na jumuiya nyingine husika. Utafiti ulifadhiliwa na Club du Sahel/DECD, CILSS na ADEA.
Kuungwa mkono na wenyeji Kwa upande mwingine, washika dau kwa sauti moja walikubaliana kuwa juhudi za programu zilifanikiwa hasa katika nyanja zilizowahusu zaidi: katika kuwawezesha watoto wenyeji "walioachwa" na shine rasmi kupata vyeti rasmi vya elimu huku wakiimarisha uwezo wao katika lugha na utamaduni wao; na katika kudhihirisha kufaa kwa lugha ya Kiafrika katika kufundishia Kifaransa na masomo mengine ya shule za msingi. Mambo yanayopendelewa katika shule ya majaribio hayana budi kuzingatiwa wakati wa kulinganisha matokeo ya aina hizi mbili za madarasa ‑ hususani upatikanaji wa vifaa vya kutosha vya kufundishia na ukweli kwamba wanafunzi wote walitoka kwenye jumuiya moja ile ile (kinyume na hali ya mchanganyiko wa wanafunzi katika shule nyingine za msingi) na walilazimika kutembea kwa miguu mwendo mrefu kila siku kufuata shule. Lakini tofauti katika safu hizi mbili za data, ambazo kusema kweli hazizingatii mtaala uliolenga mazingira ya jumuiya ambamo shule ya majaribio ilifaulu vema, zinaonyesha dhahiri kwamba mbinu za shule ya majaribio zinaweza kutoa matokeo ambayo yamelingana na yale ya shule rasmi za sasa. Profesa wa isimu aliyetajwa mapema hapo juu anafafanua zaidi: "Tunatarajia jaribio hili litasaidia kuondoa vipingamizi vya kutumia lugha za Kiafrika kwenye mfumo wetu wa elimu, ikiwa kama njia ya kufupisha muda wa masomo na pia kupanua wigo wa washiriki wa elimu ya msingi, na kama daraja jipya kati ya elimu rasmi na isiyo rasmi". " Wakati huohuo" anaongeza Profesa, "uzoefu huu vitabu vya Kifaransa vilevile vilivyokuwa vinatumiwa kwenye elimu rasmi ya shule za msingi. Zaidi ya hapo, walikuwa na shamba la mifugo lililowapatia kwenye mwaka wa masomo wa 1997 ‑ 1998 ‑ faida halisi ya faranga za CFA 233,000 (takribani $425) na walilima pia karanga na kunde kama sehemu ya mtaala wao. Hakukuwepo na waliokatisha programu, ambapo wastani wa kukatisha masomo kati ya mwaka wa kwanza na mwaka wa mwisho katika shine rasmi za msingi nchini Burkina Faso ni wa kiwango cha asilimia 40. Matokeo ya kushangaza Majaribio yaliyofanywa Desemba 1996 katika shine iliyotumia Kimoore na shine ya msingi ya jirani yalionyesha kwamba wanafunzi wa kituo cha Nomgana waliwapita wanafunzi wa shine rasmi ya msingi katika masomo ya Kifaransa na hesabu, na zaidi ya hapo, walikuwa na uelewa mzuri wa kuandika katika lugha yao ya kienyeji (ya kuzaliwa). Cha kusisimua zaidi, ni kwamba kiwango cha kufaulu cha wasichana katika kundi (ambao walikuwa wengi kidogo kuliko wavulana) kilikuwa cha juu zaidi ya kile cha wavulana wa shine rasmi ya msingi, ingawa chini ya kile cha wavulana wa kituo cha majaribio. Matokeo haya yalithibitishwa zaidi mwaka uliofuata wakati kikundi cha kwanza kutoka shine ya lugha ya Kimoore kilipofanya mtihani wa cheti cha elimu ya msingi. Viwango vya kufaulu miongoni mwa wanafunzi 53 waliofanya mtihani vilikuwa asilimia 62 kwa wavulana na asilimia 44 kwa wasichana ikilinganishwa na wastani wa kitaifa wa asilirnia 42 kwa shine zote za msingi nchini Burkina Faso (asilimia 47 katika Jimbo la Oubritenga) na kiwango kikubwa cha tofauti za kijinsia. Ingawa waratibu na viongozi wa jumuiya wanaridhika na matokeo ya hadi sasa ya programu, bado wanakabiliana na matatizo kadhaa dhidi ya juhudi zao za kutaka programu yao ilingane na ile ya shine rasmi za msingi na itoe vyeti vya diploma vinavyolingana na diploma rasmi za serikali. •
Ugumu wa kubadilika wa taratibu zilizowekwa na muda uliopangwa
kwa mambo mbalimbali yanayohitajika kwa ajili ya kuhitimu elimu
rasmi ya msingi
dhidi ya baadhi ya vipengee muhimu ambavyo kituo cha Nomgana kilikuwa
kikivifanyia majaribio ‑ kwa mfano ujumuishaji wa maarifa
ya kienyeji na "wataalam wenyeji" katika mtaala, na
kujishughulisha moja kwa moja na kilimo. "Nadharia tete yetu" anaeleza Profesa wa isimu wa Chuo Kikuu cha Ouagadougou, aliyesaidia kuandaa programu ya mafunzo haya, " ni kwamba maarifa ya lugha ya Kiafrika na matumizi ya kisomo katika lugha hiyo husaidia kwa kiwango kikubwa katika kujifunza stadi nyingine za shule ‑ kupunguza muda wa kumaliza programu ya elimu ya msingi, na kuboresha viwango vya kufaulu mitihani ya shule za msingi. Lakini programu ya Nomgana iliandaliwa kwa kuzingatia pia vipengee vingine vya shule bora. Juhudi maalum zilifanywa kujumuisha shughuli za uzalishaji mazao ya kilimo na utafiti wa utamaduni wa wenyeji katika mitaala ya masomo. Wazazi walipewa nafasi kubwa katika uongozi wa shule, na "wataalam wenyeji" ‑ hususani mafundi stadi, wanahistoria wa kimapokeo na wagani wa hadithi ‑ walialikwa kufundisha taaluma zao madarasani. Kuhudumia watoto walioachwa Awali kazi ya ufundishaji ilifanywa na vijana wa kijijini wasioajiriwa ambao walikuwa na kiwango fulani cha elimu ya sekondari, ingawa hawakuwa na uzoefu wa awali wa kufundisha. Walifundishwa mbinu za ufundishaji na wataalam wasimamizi kutoka Chuo Kikuu cha Ouagadougou. Wengi wa wanafunzi walikuwa watoto kutoka Nomgana na kijiji cha jirani cha Goue ambao walikuwa hawajajiandikisha kabisa kwenye shule ya msingi ya kijiji kwa sababu familia zao zilikuwa zimemchagua mtoto mwingine aende kusoma. Hivyo walikuwa wameshapitisha umri rasmi wa kuingia shule ya msingi (miaka 7), wakiwa na umri wa wastani wa miaka 10 walipojiunga na programu na, kwa mtazamo wa kielimu nafsia (kisiosholojia) walichukuliwa kuwa "wasingeweza kufaulu vema masomo yao". Waratibu wa programu hii walihakikisha kuwa idadi ya wasichana na wavulana waliojiunga katika programu ilikuwa sawa kabisa. Kwa ujumla, wanafunzi 55 walishiriki kwenye awamu ya kwanza, wakiwa wameganywa katika madaraka mawili, kwa uwiano wa wanafunzi ‑ mwalimu wa 25:1. wote walihitajika kupitia kwanza kisomo cha lugha ya Kimoore kwa kipindi cha miezi sita. Miaka miwili ya mwanzo masomo yalifundishwa kwa Kimoore, ingawa lugha ya Kifaransa ilifundishwa kama somo. Walipofikia mwaka wa tatu, wanafunzi walitumia. |