THE WORLD BANK GROUP A World Free of Poverty
Home

[Back to TOC]

KUTOKA "KUFURU" HADI UENDELEVU:UPANDAJI MITI UPYA NA KILIMO CHA KUTUMIA MBOLEA YA ASILI KATIKA JUMUIYA YA FORIKROM, GHANA.

Forikrom, jumuiya ya watu 6,000 katika Wilaya ya Techiman (Mkoa wa Brong Ahafo) ya Ghana, iko kwenye eneo wazi la uwanda wa nyasi ambalo wakazi wake wanadai kwamba zamani lilikuwa eneo lenye msitu mnene. Kilimo ambacho ndiyo kazi kuu, huhusu hasa mahindi, viazi vikuu, ndizi, na muhogo kwa ajili ya chakula na kuuza kwenye soko la Techiman, na kwa ajili ya biashara hulimwa mazao yafuatayo: tumbaku, michikichi, na hivi karibuni, korosho. Awali eneo lilizalisha kakao, lakini uzalishaji huo ulikoma mwaka 1983 baada ya moto kuangamiza mashamba ya mikakao. Uharibifu zaidi wa misitu ulisababishwa na mbinu mbaya za kilimo, hasa kilimo cha kisasa kilichotumika miaka ya 1960 na ambacho sasa kimeachwa, ambacho wakazi wa Forikrom wanadai kiliharibu rutuba ya udongo na kusababisha mito mikubwa na midogo kukauka.

Forikom sasa imeanza kupanda miti upya kwenye mazingira yake, lakini shughuli hü ilileta mgongano mkubwa wa kiutamaduni na ilifanikiwa to kwa kiwango kikubwa kutokana masuluhisho ya matatizo yaliyoibuliwa na mgongano wenyewe.

Mgogoro wa kidini juu ya maji Tatizo lilianza na mgogoro uliohusu matumizi ya "Asukantia," mto mdogo ambao awali daima ulikuwa ukiupatia mji maji, lakini sasa ulianza kukauka. Mto huu ulichukuliwa kuwa ni eneo takatifu na mapokeo ya muda mrefu, na ilikuwa mwiko kwenda mtoni siku za Jumanne. Mwiko huu ulizingatiwa kidini hadi mwaka 1989, kipindi kilichokuwa na ukame mkubwa nchini Ghana. Wakati wa kiangazi, madhehebu mapya katika jumuiya yalitangaza kuwa imani hiyo ilikuwa imepitwa na wakati na yakawashauri waumini wake kuuvunja mwiko huo. "Kufuru" hii mara moja ilizusha mgogoro kati ya madhehebu mapya na viongozi wa kimapokeo wa jumuiya waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa kanuni za kimila. Viongozi wa kimapokeo waliyashutumu madhehebu kwa kuikosea miungu na kusababisha kukauka kwa chanzo cha maji; nao wafuasi wa madhehebu mapya, kwa upande wao walizikana taratibu za kipagani za uongozi wa kijiji.

Mambo yalikuwa yamefikia hatua mbaya wakati kikundi cha vijana wa kiume kilipojitokeza. Vijana hawa walitaka kurejesha amani; na walikuwa pia na uelewa mpana zaidi wa masuala yahusuyo mahusiano ya kimazingira kuliko wazee wao, mathalani mahusiano kati ya uharibifu wa misitu, ukame, na kupungua kwa rutuba ya udongo.

Kikiongozwa na Katibu Msimamizi (KM) wa "Mobisquad"‑ chama cha vijana kilichoundwa chini ya Programu ya Uhamasishaji ya Kitaifa mwaka 1983 ili kuzisaidia jumuiya kuendesha programu za kustawisha maeneo yake na kupambana na majanga ya asili ‑ kikundi kilitoa pendekezo kwa jumuiya kwamba ijaribu kupanda miti kuzunguka chanzo cha mto kama njia mojawapo ya kurejesha usitawi wa mto huo. Hata hivyo, wazo hili halikuungwa mkono na Chifu na wazee, ambao walijiona wamedharauliwa na madhehebu na wakadhamiria kutatua tatizo hili kwa kufuata sheria zilizopo.

Huku kikiamini kuwa ufumbuzi wa tatizo hili ulikuwa upandaji miti kwenye chanzo cha maji, kikundi kiliamua kutekeleza chenyewe mawazo yake. Kwa bahati nzuri, kikundi kilikuwa na bahati ya kuwa na uongozi bora. Mchanganyiko wa elimu ya shuleni na uzoefu ulimwezesha KM kuwa na mtazamo wenye ubunifu zaidi wa utatuzi wa matatizo ya jumuiya . Alikuwa mhitimu wa shule ya msingi, ya kati na chuo cha ufundi stadi na alikuwa ameshahudumu katika nafasi mbalimbali za kazi kama vile mwalimu, mlipaji wa serikali katika sehemu kadhaa za Ghana na afisa mauzo nchini Nigeria. Licha ya hiyo, alikuwa pia mwinjilisti katika chama kimoja cha kimisionari. Hata hivyo, ilidhihirika punde kuwa si yeye wala wanachama wengine wa kikundi walikuwa na maarifa ya kutosha kuhusu changamoto maalum zinazoambatana na ufanikishaji wa kilimo cha miti. Kūkosekana kwa uzoefu huo miongoni mwao kulifanya iwe vigumu kuzishawishi mamlaka za kimapokeo kuwaunga mkono.

Kupata maarifa ya kuanza upya

Akitambua pingamizi hili, KM aliwashawishi wenzake kutafuta maarifa na ustadi walioukosa. Kwanza walimwendea afisa mwandamizi wa Ofisi ya Mkoa ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima iliyokuwepo Sunyani, aliyeshughulikia kazi za ugani kwenye Mkoa wa Brong Ahafo. Afisa huyo alikitembelea kijiji na kisha akakisaidia kikundi kufanya ziara.kadha kwenye Chuo cha Misitu na Idara ya Misitu ya Sunyani, kama km 100 kutoka Forikrom. Kila waliporejea nyumbani walijadiliana na jumuiya juu ya yale waliyojifunza, hasa na Chifu pamoja na wazee. Ilipofikia mwishoni mwa 1989, kikundi kilikwisha waridhisha viongozi wa kimapokeo kuwa kufungua madai mahakamani halikuwa suluhisho la matatizo ya jumuiya. Pia kikundi kilikuwa kimepata msaada wa kuanzisha mradi wa upandaji upya wa miti kutoka kwenye Chuo cha Misitu na Idara ya Misitu.

Mradi ulizinduliwa rasmi mwaka 1990 kwenye mkutano wa jumuiya ulioandaliwa na kikundi kwa kushirikiana na Ofisi ya Sunyani ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Kwenye mkutano huu, wataalam kutoka Chuo cha Misitu cha Sunyani na kutoka Ofisi za Idara ya Misitu za Sunyani na Kumasi, ambao walikuwa wakishirikiana na kikundi, walipeana zamu kufafanua juu ya umuhimu wa upandaji miti. Hususani walisisitiza matumizi ya misitu kama njia ya kuweka ukanda unaokinga eneo linalozunguka chanzo cha maji,ukanda dhidi ya dharura za hali ya hewa, ukanda wa kuzuia upepo na mioto, na pia misitu kulinda rutuba ya udongo na kutoa kuni.

Wakiwa wameridhishwa na maelezo haya, watu wazima wa jumuiya waliidhinisha wazo la kuanzisha mradi wa upandaji miti, na kisha wakashiriki katika mafunzo ya awali ya maandalizi ya vitalu vya miche yaliyoendeshwa na maofisa misitu wawili kutoka Sunyani waliotumika kama wataalam wawezeshaji na washauri. Wakati wa mfululizo wa ziara za mafunzo za saa 6 kwa kila ziara zilizoendeshwa na maofisa misitu hawa kwa kipindi cha miezi sita, vikundi vya watu thelathini thelathini vilifundishwa namna ya: kuandaa ardhi na kulima vitalu; kutunza miche; kuatika kupandikiza; na kutunza miti michanga. Jumla ya watu 2000, yaani wengi wa watu wazima wa Forikrom, walishiriki kwenye mafunzo haya.

Kwa msaada wa kiufundi kutoka kwa wataalam na msaada kidogo wa fedha kutoka kwenye mashirika kama vile Shirika la Maendeleo na Msaada la Kisabato, kikundi kilianzisha bustani ya miche, mwanzoni kwa ajili ya mradi wa upandaji miti upya na kisha kwa ajili ya biashara pia. Mikorosho, michikichi na mivule ilitolewa kwa wanajumuiya ill wakaipande kwenye mashamba yao. Hadi ilipofikia Oktoba 1993, mradi ulikuwa umegawa bure miche 15,000 kwa vikundi vingi vilivyolitembelea shamba kutoka maeneo mengine. Kwa hall hii, KM na wenzake kumi walipata maarifa ya kutosha yaliyowawezesha kuchukuliwa kuwa wawezeshaji na washauri makini. Taratibu mradi ulikua na kuwa kituo kikubwa cha elimu ya misitu ya ugani kwa maeneo yote ya karibu na Forikrom.

Mwishom mwa 1995, baada ya kuwa tayari na soko zuri la mivule, michikichi na mikorosho, spishi zenye mwelekeo mzuri wa mauzo, mradi uliamua kufanya uzalishaji na uuzaji wa miche kuwa shughuli ya biaslia~a ‑ na mwanzoni mwa 1996 mauzo ya kwanza ya michikichi yalifanywa. Mahitaji ya mivule yalielekea yangepanuka kwa vile wakulima eneoni waliendelea kupanda miti hiyo kama vizuizi vya mioto na, kwa siku za mbele ilitarajiwa mahitaji ya milingoti ya simu na umeme yangeongeza biashara ya mivule. Mintarafu mikorosho, watu wengi wa Forikrom na maeneo yanayoizunguka walipendelea kuipanda. Ndani ya jumuiya, katika miaka ya hivi karibuni wakulima wamepanda zaidi ya ekari 100, na mauzo ya korosho yamekuwa yakiongezeka kadiri mikorosho inavyozidi kupea.

Kupanua matokeo ya mradi:ulinzi wa mazingira na kilimo cha kutumia mbolea ya asili Mradi uliotokana na mgogoro juu ya vyanzo vya maji ulikuwa pia na matokeo mengine mazuri (chanya). Chama cha Kulinda Mazingira cha Forikrom (Forikrom Environmental Protection Association ‑ EPA), kilichotokana na mradi wa upandaji miti, kilipata hadhi kubwa wakati Shirika la Kulinda Mazingira la Ghana lilipotumia tawi la Forikrom kama kitovu cha kutawanyia taarifa za utunzaji mzuri wa mazingira kwa jumuiya za eneo la kati ya Techiman na Nkoranza. Kuanzia mwaka 1994 tawi la Forikrom la EPA lilikaribishwa kwenye mfululizo wa warsha juu ya uanzishaji wa vitalu vya miche na utunzaji wa miti zilizoandaliwa na shirika moja huko Kumasi. Matokeo ya warsha hizi yalichapishwa na kusambazwa kwa wenyeji, na Forikrom pole pole kikawa kituo cha mafunzo ya usimamizi wa maliasili na taaluma ya misitu kilichofadhiliwa na wahisani mbalimbali.

Jambo la pili linalotokana na mgogoro juu ya haki za maji ni kuanzishwa kwa Mradi wa Kilimo cha Kutumia Mbolea ya Asili cha Abrono (Abrono Organic Farming Project (ABOFAP). Ukiwa umebuniwa na KM na wenzake mnamo mwaka 1992, mradi ulishughulikia tatizo la upungufu wa rutuba ya udongo ambacho kilikuwa kiini cha mgogoro wa "Asukantia". Malengo yake mahususi yalikuwa kuwafundisha wakulima vijana kilimo ēha kutumia mbolea ya asili, kuhamasisha matumizi ya mboji ili kurutubisha ardhi (na kupiga vita matumizi ya kemikali), mbinu za kilimo cha kiangazi cha mbogamboga, na uzalishaji wa uyoga.

Kunako mwishoni mwa 1990, KM, akiwa na mwanamke ambaye hakuwa na ajira ‑mhitimu wa shule ya kati ‑ kutoka Forikrom, walihudhuria mafunzo ya siku tano huko Kumasi yaliyoandaliwa na Programu ya Afrika 2000. Yakijumuisha saa 12 za masomo ya darasani na saa 18 za mazoezi ya vitendo na kuangalia maonyesho mashambani, mafunzo yao yalihusu stadi za vitalu, kilimo mseto, na utayarishaji wa mboji. Uzoefu huu ulifuatiwa na kushiriki kwenye warsha nyingine na kutembelea mashamba ambako kuliimarisha maarifa yao juu ya kilimo cha kutumia mbolea ya asili.

Wakati huohuo KM alianzisha mashamba ya maonyesho kwenye ardhi yake ya Forikrom ili kuamsha ari ya kilimo cha kutumia mbolea ya asili miongoni mwa vijana. Alianza na wanamafunzo 20, 10 wanaume na 10 wanawake, wote wakiwa wahitimu wa shule wasioajiriwa wenye umri wa kati ya miaka 17 na 25. Aliwagawanya katika vikundi vya watu wanne wanne na kila kikundi kikapatiwa eneo la kufanyia kazi karibu na mto Asukantia.

llipofikia mwaka 1996, mradi wa ABOFAP ulikuwa umeshafundisha vijana 130 (75 wanaume na 55 wanawake) kilimo cha kiangazi cha bustani za mboga cha kutumia mbolea ya asili, wengi wao wakiwa wahitimu wa shine ya kati walioishi na wazazi wao. Miezi mitatu ya mafunzo waliyoipata vijana hawa iliwafungulia mlango muhimu wa kujiajiri wenyewe. Kwenye mzunguko wa miezi mitatu ya kwanza, kwa mfano, kikundi cha awali cha vijana 20 kilizalisha pato la c200,000, au $355, kutokana na mauzo ya mbogamboga, na wakagawana sawasawa pato halisi la c 160,000, au $308 (kiwango cha kubadilisha fedha kwa Desemba 1992 kilikizwa c519 = $1.00).

Ukitoa takribani asilimia 10 ya wahitimu wa mafunzo haya walioona kilimo kuwa kazi ngumu na hivyo kukiacha, washiriki wengine wote sasa wanajitegemea na wana mafanikio mazuri. Wahitimu wa awali wanajishughulisha na kilimo cha korosho na wana matarajio mazuri kwa siku za baadaye. Karibu vijana 200 wamejiunga katika vyama vya ushirika vya watu 6 hadi 10 ili kulima kwa bloku za ekari 1 ‑ 2 pembezoni mwa mto.

Cha kushangaza ni kwamba KM hakuchukua nafasi ya uongozi wa juu kwenye mashirika aliyoyaanzisha ama aliyoyalea. Badala yake amewashawishi watu wengine kushiriki katika uongozi. Kwa mfano, mkulima mzee asiye na kisomo ndiye Rais wa Mradi wa Upandaji miti wa Forikrom wenye wanachama 2000, huku KM akihudumu kama Katibu, na pamoja na watu wengine watatu kama mjumbe wa Kamati ya Utendaji. Vivyo hivyo, mkulima mzee wa miaka 60 mwenye Cheti cha Kumaliza Shule ya Kati, ndiye Rais wa Chama cha Kulinda Mazingira cha Forikrom chenye wanachama 90. Na kijana wa miaka 23 aliye mhitimu wa shule ya sekondari, huhudumu kama Katibu wa Mradi wa ABOFAP wenye wanachama 20.

Kufanya amani na jumuiya na mazingira

Maendeleo makubwa yamefanyika Forikrom katika kipindi cha chini ya muongo mmoja. Vyanzo vipya vya kuingizia mali vimebuniwa na kuendelezwa. Lakini matokeo muhimu zaidi ya miradi ya Forikrom yanahusiana na ubora wake. Tokeo la kwanza ni uhusiano mzuri wa kijamii. Mgawanyiko wa jumuiya uliopandikizwa na mgogoro kati ya madhehebu na viongozi wa kimapokeo ulikwisha baada ya jumuiya nzima kushiriki kupanda miti iliyokinga chanzo cha mto Asukantia. Msisimko wa jumuiya juu ya upandaji miti, mazao mapya ya biashara, zana bora za kilimo, na kutambuliwa kwa kazi za jumuiya na taasisi za nje kumemfanya kila mtu kusahau mgogoro uliowatenganisha hapo awali.

Jambo jingine muhimu ni uanzishwaji wa jumuiya inayojali mazingira ambayo huonekana kama mfano wa kuigwa na miji mingine katika mkoa. Katika kipindi cha miaka sita iliyopita ukanda ‑zuizi wa ekari 4 za mivule na ekari 3 za "leucenea" umeoteshwa kuzunguka chanzo na mto wa Asukantia. Sasa kuna maji yakutosha mtoni, kiasi cha kwamba wakati mwingine watu huyatumia kwa ajili ya kilimo cha kiangazi cha mbogamboga. Zaidi ya hapo, viongozi wa kijiji wanaripoti kuwa wananchi hawachomi ovyo tena misitu na, kutokana na hali hiyo, hakujawa na mioto ya misituni tangu mwaka 1990.

Msingi wa makala hii ni utafiti uliofanywa na watafiti kutoka Ghana, Kanada na Marekani kwa msaada na ushauri wa kiufundi wa Prof Peter Easton wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Florida, wakishiriana na jumuiya nyingine husika. Utafiti ulifadhiliwa na Club du Sahel OECD, CILSS na ADEA.


[Back to TOC]


Footer