|
Uvumbuzi
upya wa Uanagenzi na Taratibu za Kuingia Utu Uzima: Kuingia kwenye
Uchumi – miji katika Afrika Kusini mwa Sahara Jamii
nyingi za kimapokeo katika Afrika Kusini mwa Sahara zina mifumo mizuri
ya kuwaingiza vijana katika desturi, stadi na uelewa wa utu uzima. Mifumo hiyo hujumuisha vyama vya marika,
unyago na jando, na uanagenzi katika stadi mbalimbali za uzalishaji
mali. Kizazi
Kilichoachwa Kifanye Kipendavyo
Kwa
ujumla, uhamiaji mijini kutoka vijijini umechangia katika kuvunja
polepole uhusiano na nguvu za mila za jando na unyago na utaratibu
wa uanagenzi tangu upatikane “uhuru wa bendera”. Mfano wa upeo wa
uvunjaji wa desturi hizi za kuingia utu uzima pengine unaonyeshwa
na hali ya watoto wa mitaani, wale vijana wasio na elimu, kazi na
aghalabu makazi ya kudumu ambao wanazurura katika barabara kuu na
ndogo za miji ya Afrika. Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na ‘NGO’ nyingi zinazoshughulikia suala hili huwachukulia
watoto wa mitaani kama kikundi cha watoto wanaofanya kazi – yaani,
watoto wadogo ambao hawajafikia umri
rasmi wa kuajiriwa au hawajakomaa kijamii ambao wanafanya kazi
katika mazingira yenye kuleta madhara katika makuzi na maendeleo yao.
Watoto wengi katika jamii zinazoendelea, ni kweli, kuwa wanafanya
kazi na wataendelea kufanya kazi. Changamoto
iliyo sahihi zaidi sio kukataza aina zote za kazi kwa watoto wenye
umri mdogo, bali kuhakikisha kwamba watoto hawalazimishwi kufanya
kazi zisizofaa na za hatari kwa sababu ya kuokoa maisha yao, na kwamba
wapatiwe fursa nzuri za kuingia katika maisha ya utu uzima. Lakini hali mbaya ya watoto wa mitaani inadokeza hali ya uchumi ilivyo pembezoni mwa miji, ambako ukosefu wa fursa za kijamii umewanyima vijana wakimbizi nafasi ya kukuza utambulisho wa utu uzima. Miundo ya kimapokeo ya jamii si rahisi kujitokeza sasa. Kama methali ya Kihausa inayosema “In rawa ta sake, ki’di ita ma sai ta sake”: Mdundo wa ngoma unapobadilika, uchezaji wa ngoma pia hubadilika. Ipi ni midundo mipya ya maana katika mazingira ya sasa ya kiuchumi na kiutamaduni, na kadhalika hali iliyobadilika inayoitia changamoto midundo hiyo? Mifano mitatu kutoka Afrika na mmoja kutoka Caribbean inatoa mwangaza kwa kiasi fulani. Mwaka
1973, padri alianza kutumia muda wake mwingi mitaani akijenga uhusiano
mwema na watoto wa mitaani na kuzungumza nao kuhusu hali halisi ya
maisha yao na juu ya matarajio yao. Aligundua kuwa wengi wao walikuwa
wameacha shule za msingi na kuhama toka nyumbani kwao kwa sababu familia
zao hazikuweza kuwalipia karo za shule na kuwanunulia sare na vifaa
vinginevyo vya shule. Wengi wao, kama kiongozi mmoja wa Chama cha
Undugu anavyoeleza, walipoulizwa wanahitaji nini, walijibu “Nataka
kusoma”. Kutokana
na sababu hizi, awali padri aliamua kwamba jitihada za kuwasaidia
watoto wa mitaani zielekezwe zaidi katika kuwarejesha shuleni, na
akaanza kutafuta fedha za kulipia karo na vifaa vingine vya shule
kwa vijana wengi kadiri ilivyowezekana. Hata hivyo, aligundua punde
kuwa mara nyingi wakuu wa shule waliwakataa watoto hao au hawakutaka
warejee kwenye shule zao za awali. Wakuu hao walihofu kuwa sababu
zilezile zilizowafanya watoto hawa watoroke shule mara ya kwanza zinaweza
zikajirudia; ama kutokana na tabia zilizojengwa huko mitaani, watoto
hawa hawawezi kuendana na utaratibu wa kawaida wa shule. Namna
ya kujifunza
Matatizo
haya ya kwanza yalifuatiwa na mikakati mbalimbali ambayo hatimaye
ilikiwezesha Chama cha Undugu kubuni mkabala wenye mafanikio zaidi
uliokidhi hali ya vijana masikini wa Nairobi. Mkabala huo ulikuwa
na hatua nne. Hatua ya kwanza ilikuwa mtandao wa “shule zisizo rasmi”
zilizoenezwa katika makazi ya watu masikini ndani na pembezoni mwa
jiji la Nairobi. Shule hizi zililenga wavulana na wasichana wenye
umri wa miaka 10 – 16 ambao walikuwa hawajaenda shule kabisa ama ambao
walishindwa kuendelea na shule, na hivyo kuwa katika hatari ya kuwa
watoto wa mitaani wafanyakazi, kama kweli walikuwa hawajawa hivyo
tayari. Programu hii ilipangwa ichukue miaka mitatu, iwapatie washiriki
elimu ya msingi (kusoma na kuandika) na stadi za kunusuru maisha,
pia iwawezeshe kujithamini, na hali kadhalika iwawezeshe wale wanaohitaji
kurudi kwenye utaratibu rasmi wa elimu au kujiunga na vyuo vya ufundi
stadi. Kurejea
huku kwenye elimu rasmi au mafunzo ya ufundi stadi ndiyo ilikuwa hatua
ya pili ya mkabala na ilichukua mwaka mmoja zaidi. Wale waliobaki
kwenye programu hii – au wale waliorejea baada ya kumaliza shule rasmi
– walipata nafasi ya kujaribu ujuzi wao katika kazi mashuhuri za ufundi
za sekta ya uchumi isiyo rasmi za Nairobi: hususani ufundi seremala,
ushonaji, ufundi magari na ufundi chuma. Kwa kazi zote hizi Chama
cha Undugu kilikuwa na zana za kutosha za kufanyia kazi kwenye karakana
yake. Hatua
ya tatu ilijumuisha kipindi cha mpito kuelekea katika ajira na majukumu
ya kiuchumi ya utu uzima. Vijana walioonyesha upendeleo wa kazi ya
ufundi mahususi walisaidiwa kumpata fundi stadi katika sekta isiyo
rasmi ambaye angewachukua kama wanagenzi kwa kipindi cha mwaka mmoja
ili wapate mafunzo zaidi na uzoefu. Chama cha Undugu kilishiriki kama
mwenzi katika mapatano haya na kikabuni vigezo vya kuteua mafundi
stadi “ wenyeji” na taratibu za ukaguzi wa mara kwa mara wa vifaa
vya Chama ili kuhakikisha kuwa wanagenzi wanafundishwa na kwamba mazingira na masharti ya kazi si
ya kinyonyaji. Wakati wa mwaka huu wa uanagenzi, vijana walirejea
kwenye karakana za Makao Makuu ya Undugu kila juma ili “kuinua viwango
vya stadi zao”. Mafunzo haya yalihusu hasa matumizi ya zana za kazi
ambazo mafundi stadi wengi hawakuweza kuyafundisha, na wakati huo
huo yalilenga kuwatayarisha vijana kufanya mitihani ya kwanza ya serikali
ya ufundi stadi kwenye stadi walizochagua. Mitihani hii ilifanyika
mwishoni mwa mwaka. Kuwapatia
nafasi za kazi wahitimu wa Undugu, au kuwawezesha kujiajiri wenyewe
kwa faida kwenye sekta isiyo rasmi ndiyo ilikuwa hatua ya mwisho na
ya nne. Kitengo cha Ushauri wa Kibiashara cha Undugu hutoa mafunzo
ya kuanzisha miradi midogo midogo na mikopo kwa wahitimu wa programu
ili kuwasaidia wajiimarishe kwenye kazi zao. Chama vilevile kimeanzisha
Idara ya Usanifu na uuzaji wa bidhaa na huduma zinazotolewa na sekta
isiyo rasmi na hasa katika kazi za ufundi zinazosaidiwa na Undugu
na zinazofanywa na mafundi stadi walio na wanagenzi wa Undugu. Wafanyakazi
wa Kitengo cha Usanifu Viwanda huendesha warsha kwa mafundi stadi
wa sekta isiyo rasmi wanaoshirikiana na Undugu juu ya usanifu na uuzaji
wa mazao yao. Kwa kufanya hivyo huwatumia wanagenzi wa Undugu kama
nyenzo ya kuboresha mazao yanayotolewa na sekta isiyo rasmi. Mikabala Mingine Mbalimbali Huduma
ya Uchukuzi ya Watoto wa Mitaani mjini Khartoum
Mkabala
tofauti lakini unaohusiana (na ule wa Nairobi) umechukuliwa na shirika
lisilo la kiserikali (NGO) – Shirika la Kimataifa la Watoto wa Mitaani
(SKWM) linalofanya kazi Khartoum, Sudan (kwa lugha ya kiingereza shirika
hili huitwa Street Kids International – SKI). Tatizo la jinsi ya kuwaingiza
vijana hawa katika jamii ya mjini na uchumi wa mjini liliwafanya watumishi
wa shirika pamoja na vijana wenyewe kutafakari juu ya “unafuu wa kiuchumi”
walionao watoto wa mitaani katika soko la mjini. Moja ya stadi zao
ni kwamba wanaifahamu vema mitaa – yaani, barabara kuu na ndogo za
jiji unganifu la Khartoum, na pia wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi
katika mazingira ambayo yangewatisha watu wengine. Watumishi na watoto
wa mitaani walizingatia ukweli huu dhidi ya kile wachumi wanachokiita
sasa “mambo magumu” katika uchumi wa mijini, na hususani ugumu wa
kusafirisha vifurushi na vifaa vinginevyo kutoka sehemu moja hadi
nyingine ya jiji la Khartoum lenye msongamano wa magari. Ndipo wakaja
na wazo la kuanzisha Huduma ya Uchukuzi ya Watoto wa Mitaani. Mpango
huu ulijumuisha mambo yafuatayo: ·
Kukopa baiskeli
kwa wachukuzi, ambapo baadaye kila mtoto angelipia mkopo huo kutokana
na ujira wake wa kazi. ·
Kuwafunza
watoto taratibu za uchukuzi na hatua za usalama. ·
Kuwasaidia
kuanzisha mpangilio mzuri wa ufanyaji kazi na utunzaji wa mahesabu
utakaoufanya mradi utekelezeke. Kwa
hakika mradi ulikuwa na mafanikio ya kutosha; na mfano wake uliigwa
na Shirika la Kimataifa la Watoto wa Mitaani la Banglore, nchini India,
miaka michache baadaye. Chama cha Mafundi Stadi cha Senegal
(ENDA/GRAF) Kutokana
na hali hii, vyama viliamua kuanzisha mfumo wake wa uanagenzi ili
kuwawezesha vijana wajuane katika sehemu zao za kazi na waingie vizuri
kwenye maisha ya utu uzima. Ushirika wa maseremala ndio ulikuwa msitari
wa mbele kabisa katika suala hili na ulibuni mfumo wa kuwazungusha
vijana walioacha shule na kuchukuliwa kama wanagenzi wa Ushirika kwa
mafundi stadi mbalimbali ambako walijifunza stadi za kazi tofautitofauti,
na kisha – kwa msaada wa ENDA/GRAF – wakafundishwa pia utunzaji fedha
na uongozi wa miradi midogomidogo. SERVOL nchini Trinidad. Mfano wa mwisho unachukuliwa mahali palipo mbali
kabisa na bara la Afrika, lakini panafungamana na bara hilo kwa njia
nyingi za kihistoria na kiutamaduni: yaani kisiwa cha Trinidad huko
West Indies. Matatizo ya mpito wa vijana kuelekea ukubwani katika
mazingira ya mijini ni makubwa kama vile ilivyoonekana kwenye mifano
mitatu tulioijadili hivi punde – na kwa namna fulani, chanzo cha programu
mashuhuri inayoshughulikia matatizo hayo, SERVOL (Service Volunteered
for All” – Huduma Inayoletwa Bure kwa Wote) kimefanana pia. Kama Chama
cha Undugu, SERVOL ilianzishwa na padri wa Kikatoliki aliyechukizwa
na hali duni ya vijana mjini. Kama
Undugu, SERVOL kimekuwa chama ambacho sio tu kinatoa ajira bali pia
hutoa njia mbadala za vijana kufahamiana wanapoingia katika maisha
ya utu uzima. Miongoni mwa njia hizo ni “Vituo vya Maisha” vya SERVOL. Kama
jina linavyoashiria, Vituo vya Maisha ni zaidi ya kuwa fursa za kufunzia
ufundi stadi. Kwanza kabisa vituo hivi hujengwa na vijana wakubwa
ili kupata majengo ya karakana, madarasa na huduma nyingine za kijumuiya.
Pia kila kituo hutumika kama kituo cha chekechea, na washiriki wote
hupangiwa majukumu ya kuwaangalia watoto wadogo au chekechea hao.
Kisha mkazo pia huwekewa ushauri nasaha wa marika na kutoa fursa kwa
vijana kueleza matatizo yao ya kijamii na yanayotokana na jazba za
ujana huku wakizingatia maadili ya dini kuu tatu za kisiwani mwao:
Ukristo, Uislamu na Uhindu. Vijana hushiriki katika kuandaa mtaala
wao maalum unaojumuisha uelewa wa kiroho, kimwili, kiakili, kiutamaduni
na kimhemko. Kutoka hapo, washiriki huweza kuingia kwenye vyuo vya
ufundi stadi na kuajiriwa au kuwa na sifa za kupatiwa mikopo midogo
ya kuanzishia miradi yao binafsi. Kiwango cha vijana wanaoshindwa
kuendelea na programu hii ni asilimia 5 tu, ambapo kiwango cha kuajiriwa
au kujiajiri baada ya kufuzu mafunzo ya stadi mbalimbali ni asilimia
75. Viambato
muhimu:ajira, maana na kujiongoza Mafundisho
mengine machache yanajitokeza kutokana na juhudi za kuwasaidia vijana
masikini wa Afrika kujenga utambulisho mpya: ·
Mkabala
wa “elimu ya watu wazima” hufanikiwa vizuri iwapo utajengwa juu ya
uzoefu na stadi walizonazo tayari vijana na kuwapatia nafasi ya kuchangia
kutoa maamuzi ya kuendesha programu husika. ·
Ajira yenye
faida ni msingi wa utambulisho mpya, lakini sio wa mshikamano. Mshikamano
huletwa na kuwepo kwa mpango wa maendeleo wa muda mrefu mbele – uwe
wa kidini, kiutamaduni ama kisiasa – na fursa ya kuutumia katika maisha
ya mtu binafsi. Hivyo ushauri nasaha wa marika mara nyingi ni jambo
muhimu la kufanikisha programu. ·
Namna za
kimapokeo za uanagenzi na vyama vya vijana zafaa zitumike kama rasilimali
za kusonga mbele kimaendeleo, pia lazima zihakikiwe. Programu za namna
hiyo huwa kama uwanja wa majaribio kwa tamaduni nyingi za jirani. ·
Utambuzi
wa mazingira yanayomzunguka mtu – na haja ya kuyabadili – ni vijalizo
muhimu vya juhudi zozote zile. *msingi
wa makala hii ni utafiti uliofanywa na watafiti wenyeji kwa msaada
na ushauri wa kiufundi wa Prof. Peter Easton wa Chuo Kikuu cha Jimbo
la Florida, wakishirikiana na baadhi ya jumuiya za Kiafrika. Utafiti
ulifadhiliwa na Club du Sahel/OECD, CLISS na ADEA. Jamii
nyingi za kimapokeo katika Afrika Kusini mwa Sahara zina mifumo mizuri
ya kuwaingiza vijana katika desturi, stadi na uelewa wa utu uzima. Mifumo hiyo hujumuisha vyama vya marika,
unyago na jando, na uanagenzi katika stadi mbalimbali za uzalishaji
mali. Utaratibu
wa kimapokeo kwa ajili ya uanagenzi na jando na unyago bado una mashiko
katika jumuiya za vijiji ilihali unalegalega kwenye maeneo ya pembezoni
mwa miji miongoni mwa watu ambao njaa, ukosefu wa ajira au mvuto wa
maisha mazuri zaidi umewafanya wakimbilie mijini. Hapana shaka kuna
mambo mbalimbali yanayounganisha maeneo haya mawili, na vyama vya
wahamiaji kutoka vijiji na mikoa mbalimbali ni mambo ya kawaida mijini. Kizazi
Kilichoachwa Kifanye Kipendavyo
Kwa
ujumla, uhamiaji mijini kutoka vijijini umechangia katika kuvunja
polepole uhusiano na nguvu za mila za jando na unyago na utaratibu
wa uanagenzi tangu upatikane “uhuru wa bendera”. Mfano wa upeo wa
uvunjaji wa desturi hizi za kuingia utu uzima pengine unaonyeshwa
na hali ya watoto wa mitaani, wale vijana wasio na elimu, kazi na
aghalabu makazi ya kudumu ambao wanazurura katika barabara kuu na
ndogo za miji ya Afrika. Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na ‘NGO’ nyingi zinazoshughulikia suala hili huwachukulia
watoto wa mitaani kama kikundi cha watoto wanaofanya kazi – yaani,
watoto wadogo ambao hawajafikia umri
rasmi wa kuajiriwa au hawajakomaa kijamii ambao wanafanya kazi
katika mazingira yenye kuleta madhara katika makuzi na maendeleo yao.
Watoto wengi katika jamii zinazoendelea, ni kweli, kuwa wanafanya
kazi na wataendelea kufanya kazi. Changamoto
iliyo sahihi zaidi sio kukataza aina zote za kazi kwa watoto wenye
umri mdogo, bali kuhakikisha kwamba watoto hawalazimishwi kufanya
kazi zisizofaa na za hatari kwa sababu ya kuokoa maisha yao, na kwamba
wapatiwe fursa nzuri za kuingia katika maisha ya utu uzima. Lakini
hali mbaya ya watoto wa mitaani inadokeza hali ya uchumi ilivyo pembezoni
mwa miji, ambako ukosefu wa fursa za kijamii umewanyima vijana wakimbizi
nafasi ya kukuza utambulisho wa utu uzima. Miundo ya kimapokeo ya
jamii si rahisi kujitokeza sasa. Kama methali ya Kihausa inayosema
“In rawa ta sake, ki’di ita ma sai ta sake”: Mdundo wa ngoma unapobadilika,
uchezaji wa ngoma pia hubadilika. Ipi ni midundo mipya ya maana katika
mazingira ya sasa ya kiuchumi na kiutamaduni, na kadhalika hali iliyobadilika
inayoitia changamoto midundo hiyo? Mifano mitatu kutoka Afrika na
mmoja kutoka Caribbean inatoa mwangaza kwa kiasi fulani. Kusimamisha wimbi la watoto wa mitaani:
Chama cha Undugu cha Kenya Chama
cha Undugu kilianzishwa kwa juhudi za padri mmoja wa Kiholanzi aliyehamia
Nairobi mwaka 1972 baada ya uzoefu wa miaka 17 ya kuishi vijijini
nchini Tanzania, ambako alianzisha huduma za kichungaji kwa vijana
wa mijini. Vijana wachache waliziitikia programu zake za kidini, lakini
aliona kwamba mitaa ya Nairobi ilifurika vijana wasio na ajira, hasa
vijana “waegeshaji magari” ambao waliomba ujira kidogo kutoka kwa
wenye magari kwa ajili ya kuyalinda na kuyaosha magari hayo katikati
ya jiji la Nairobi lenye msongamano wa watu na vitu. Mwaka
1973, padri alianza kutumia muda wake mwingi mitaani akijenga uhusiano
mwema na watoto wa mitaani na kuzungumza nao kuhusu hali halisi ya
maisha yao na juu ya matarajio yao. Aligundua kuwa wengi wao walikuwa
wameacha shule za msingi na kuhama toka nyumbani kwao kwa sababu familia
zao hazikuweza kuwalipia karo za shule na kuwanunulia sare na vifaa
vinginevyo vya shule. Wengi wao, kama kiongozi mmoja wa Chama cha
Undugu anavyoeleza, walipoulizwa wanahitaji nini, walijibu “Nataka
kusoma”. Kutokana
na sababu hizi, awali padri aliamua kwamba jitihada za kuwasaidia
watoto wa mitaani zielekezwe zaidi katika kuwarejesha shuleni, na
akaanza kutafuta fedha za kulipia karo na vifaa vingine vya shule
kwa vijana wengi kadiri ilivyowezekana. Hata hivyo, aligundua punde
kuwa mara nyingi wakuu wa shule waliwakataa watoto hao au hawakutaka
warejee kwenye shule zao za awali. Wakuu hao walihofu kuwa sababu
zilezile zilizowafanya watoto hawa watoroke shule mara ya kwanza zinaweza
zikajirudia; ama kutokana na tabia zilizojengwa huko mitaani, watoto
hawa hawawezi kuendana na utaratibu wa kawaida wa shule. Namna
ya kujifunza
Matatizo
haya ya kwanza yalifuatiwa na mikakati mbalimbali ambayo hatimaye
ilikiwezesha Chama cha Undugu kubuni mkabala wenye mafanikio zaidi
uliokidhi hali ya vijana masikini wa Nairobi. Mkabala huo ulikuwa
na hatua nne. Hatua ya kwanza ilikuwa mtandao wa “shule zisizo rasmi”
zilizoenezwa katika makazi ya watu masikini ndani na pembezoni mwa
jiji la Nairobi. Shule hizi zililenga wavulana na wasichana wenye
umri wa miaka 10 – 16 ambao walikuwa hawajaenda shule kabisa ama ambao
walishindwa kuendelea na shule, na hivyo kuwa katika hatari ya kuwa
watoto wa mitaani wafanyakazi, kama kweli walikuwa hawajawa hivyo
tayari. Programu hii ilipangwa ichukue miaka mitatu, iwapatie washiriki
elimu ya msingi (kusoma na kuandika) na stadi za kunusuru maisha,
pia iwawezeshe kujithamini, na hali kadhalika iwawezeshe wale wanaohitaji
kurudi kwenye utaratibu rasmi wa elimu au kujiunga na vyuo vya ufundi
stadi. Kurejea
huku kwenye elimu rasmi au mafunzo ya ufundi stadi ndiyo ilikuwa hatua
ya pili ya mkabala na ilichukua mwaka mmoja zaidi. Wale waliobaki
kwenye programu hii – au wale waliorejea baada ya kumaliza shule rasmi
– walipata nafasi ya kujaribu ujuzi wao katika kazi mashuhuri za ufundi
za sekta ya uchumi isiyo rasmi za Nairobi: hususani ufundi seremala,
ushonaji, ufundi magari na ufundi chuma. Kwa kazi zote hizi Chama
cha Undugu kilikuwa na zana za kutosha za kufanyia kazi kwenye karakana
yake. Hatua
ya tatu ilijumuisha kipindi cha mpito kuelekea katika ajira na majukumu
ya kiuchumi ya utu uzima. Vijana walioonyesha upendeleo wa kazi ya
ufundi mahususi walisaidiwa kumpata fundi stadi katika sekta isiyo
rasmi ambaye angewachukua kama wanagenzi kwa kipindi cha mwaka mmoja
ili wapate mafunzo zaidi na uzoefu. Chama cha Undugu kilishiriki kama
mwenzi katika mapatano haya na kikabuni vigezo vya kuteua mafundi
stadi “ wenyeji” na taratibu za ukaguzi wa mara kwa mara wa vifaa
vya Chama ili kuhakikisha kuwa wanagenzi wanafundishwa na kwamba mazingira na masharti ya kazi si
ya kinyonyaji. Wakati wa mwaka huu wa uanagenzi, vijana walirejea
kwenye karakana za Makao Makuu ya Undugu kila juma ili “kuinua viwango
vya stadi zao”. Mafunzo haya yalihusu hasa matumizi ya zana za kazi
ambazo mafundi stadi wengi hawakuweza kuyafundisha, na wakati huo
huo yalilenga kuwatayarisha vijana kufanya mitihani ya kwanza ya serikali
ya ufundi stadi kwenye stadi walizochagua. Mitihani hii ilifanyika
mwishoni mwa mwaka. Kuwapatia
nafasi za kazi wahitimu wa Undugu, au kuwawezesha kujiajiri wenyewe
kwa faida kwenye sekta isiyo rasmi ndiyo ilikuwa hatua ya mwisho na
ya nne. Kitengo cha Ushauri wa Kibiashara cha Undugu hutoa mafunzo
ya kuanzisha miradi midogo midogo na mikopo kwa wahitimu wa programu
ili kuwasaidia wajiimarishe kwenye kazi zao. Chama vilevile kimeanzisha
Idara ya Usanifu na uuzaji wa bidhaa na huduma zinazotolewa na sekta
isiyo rasmi na hasa katika kazi za ufundi zinazosaidiwa na Undugu
na zinazofanywa na mafundi stadi walio na wanagenzi wa Undugu. Wafanyakazi
wa Kitengo cha Usanifu Viwanda huendesha warsha kwa mafundi stadi
wa sekta isiyo rasmi wanaoshirikiana na Undugu juu ya usanifu na uuzaji
wa mazao yao. Kwa kufanya hivyo huwatumia wanagenzi wa Undugu kama
nyenzo ya kuboresha mazao yanayotolewa na sekta isiyo rasmi. Mikabala Mingine Mbalimbali Huduma
ya Uchukuzi ya Watoto wa Mitaani mjini Khartoum
Mkabala
tofauti lakini unaohusiana (na ule wa Nairobi) umechukuliwa na shirika
lisilo la kiserikali (NGO) – Shirika la Kimataifa la Watoto wa Mitaani
(SKWM) linalofanya kazi Khartoum, Sudan (kwa lugha ya kiingereza shirika
hili huitwa Street Kids International – SKI). Tatizo la jinsi ya kuwaingiza
vijana hawa katika jamii ya mjini na uchumi wa mjini liliwafanya watumishi
wa shirika pamoja na vijana wenyewe kutafakari juu ya “unafuu wa kiuchumi”
walionao watoto wa mitaani katika soko la mjini. Moja ya stadi zao
ni kwamba wanaifahamu vema mitaa – yaani, barabara kuu na ndogo za
jiji unganifu la Khartoum, na pia wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi
katika mazingira ambayo yangewatisha watu wengine. Watumishi na watoto
wa mitaani walizingatia ukweli huu dhidi ya kile wachumi wanachokiita
sasa “mambo magumu” katika uchumi wa mijini, na hususani ugumu wa
kusafirisha vifurushi na vifaa vinginevyo kutoka sehemu moja hadi
nyingine ya jiji la Khartoum lenye msongamano wa magari. Ndipo wakaja
na wazo la kuanzisha Huduma ya Uchukuzi ya Watoto wa Mitaani. Mpango
huu ulijumuisha mambo yafuatayo: ·
Kukopa baiskeli
kwa wachukuzi, ambapo baadaye kila mtoto angelipia mkopo huo kutokana
na ujira wake wa kazi. ·
Kuwafunza
watoto taratibu za uchukuzi na hatua za usalama. ·
Kuwasaidia
kuanzisha mpangilio mzuri wa ufanyaji kazi na utunzaji wa mahesabu
utakaoufanya mradi utekelezeke. Kwa
hakika mradi ulikuwa na mafanikio ya kutosha; na mfano wake uliigwa
na Shirika la Kimataifa la Watoto wa Mitaani la Banglore, nchini India,
miaka michache baadaye. Chama cha Mafundi Stadi cha Senegal
(ENDA/GRAF) Kutokana
na hali hii, vyama viliamua kuanzisha mfumo wake wa uanagenzi ili
kuwawezesha vijana wajuane katika sehemu zao za kazi na waingie vizuri
kwenye maisha ya utu uzima. Ushirika wa maseremala ndio ulikuwa msitari
wa mbele kabisa katika suala hili na ulibuni mfumo wa kuwazungusha
vijana walioacha shule na kuchukuliwa kama wanagenzi wa Ushirika kwa
mafundi stadi mbalimbali ambako walijifunza stadi za kazi tofautitofauti,
na kisha – kwa msaada wa ENDA/GRAF – wakafundishwa pia utunzaji fedha
na uongozi wa miradi midogomidogo. SERVOL nchini Trinidad. Mfano wa mwisho unachukuliwa mahali palipo mbali
kabisa na bara la Afrika, lakini panafungamana na bara hilo kwa njia
nyingi za kihistoria na kiutamaduni: yaani kisiwa cha Trinidad huko
West Indies. Matatizo ya mpito wa vijana kuelekea ukubwani katika
mazingira ya mijini ni makubwa kama vile ilivyoonekana kwenye mifano
mitatu tulioijadili hivi punde – na kwa namna fulani, chanzo cha programu
mashuhuri inayoshughulikia matatizo hayo, SERVOL (Service Volunteered
for All” – Huduma Inayoletwa Bure kwa Wote) kimefanana pia. Kama Chama
cha Undugu, SERVOL ilianzishwa na padri wa Kikatoliki aliyechukizwa
na hali duni ya vijana mjini. Kama
Undugu, SERVOL kimekuwa chama ambacho sio tu kinatoa ajira bali pia
hutoa njia mbadala za vijana kufahamiana wanapoingia katika maisha
ya utu uzima. Miongoni mwa njia hizo ni “Vituo vya Maisha” vya SERVOL. Kama
jina linavyoashiria, Vituo vya Maisha ni zaidi ya kuwa fursa za kufunzia
ufundi stadi. Kwanza kabisa vituo hivi hujengwa na vijana wakubwa
ili kupata majengo ya karakana, madarasa na huduma nyingine za kijumuiya.
Pia kila kituo hutumika kama kituo cha chekechea, na washiriki wote
hupangiwa majukumu ya kuwaangalia watoto wadogo au chekechea hao.
Kisha mkazo pia huwekewa ushauri nasaha wa marika na kutoa fursa kwa
vijana kueleza matatizo yao ya kijamii na yanayotokana na jazba za
ujana huku wakizingatia maadili ya dini kuu tatu za kisiwani mwao:
Ukristo, Uislamu na Uhindu. Vijana hushiriki katika kuandaa mtaala
wao maalum unaojumuisha uelewa wa kiroho, kimwili, kiakili, kiutamaduni
na kimhemko. Kutoka hapo, washiriki huweza kuingia kwenye vyuo vya
ufundi stadi na kuajiriwa au kuwa na sifa za kupatiwa mikopo midogo
ya kuanzishia miradi yao binafsi. Kiwango cha vijana wanaoshindwa
kuendelea na programu hii ni asilimia 5 tu, ambapo kiwango cha kuajiriwa
au kujiajiri baada ya kufuzu mafunzo ya stadi mbalimbali ni asilimia
75. Mafundisho
mengine machache yanajitokeza kutokana na juhudi za kuwasaidia vijana
masikini wa Afrika kujenga utambulisho mpya: ·
Mkabala
wa “elimu ya watu wazima” hufanikiwa vizuri iwapo utajengwa juu ya
uzoefu na stadi walizonazo tayari vijana na kuwapatia nafasi ya kuchangia
kutoa maamuzi ya kuendesha programu husika. ·
Ajira yenye
faida ni msingi wa utambulisho mpya, lakini sio wa mshikamano. Mshikamano
huletwa na kuwepo kwa mpango wa maendeleo wa muda mrefu mbele – uwe
wa kidini, kiutamaduni ama kisiasa – na fursa ya kuutumia katika maisha
ya mtu binafsi. Hivyo ushauri nasaha wa marika mara nyingi ni jambo
muhimu la kufanikisha programu. ·
Namna za
kimapokeo za uanagenzi na vyama vya vijana zafaa zitumike kama rasilimali
za kusonga mbele kimaendeleo, pia lazima zihakikiwe. Programu za namna
hiyo huwa kama uwanja wa majaribio kwa tamaduni nyingi za jirani. ·
Utambuzi
wa mazingira yanayomzunguka mtu – na haja ya kuyabadili – ni vijalizo
muhimu vya juhudi zozote zile. *msingi
wa makala hii ni utafiti uliofanywa na watafiti wenyeji kwa msaada
na ushauri wa kiufundi wa Prof. Peter Easton wa Chuo Kikuu cha Jimbo
la Florida, wakishirikiana na baadhi ya jumuiya za Kiafrika. Utafiti
ulifadhiliwa na Club du Sahel/OECD, CLISS na ADEA. |