Senegal:
Demokrasia ya Umma ikifanya kazi
Demokrasia kuanzia kwenye familia
hadi kwenye ngazi ya Taifa Kabla
ya kuandaa maudhui mapya, wafanyakazi wa NGO waliamua kufanya utafiti
uliowashirikisha wananchi ili kujua mahitajio muhimu ya wananchi hao
katika mafunzo ambayo yangetolewa. Matokeo ya utafiti yalikuwa ya
kushangaza. Wananchi walihitaji sana kupanua uelewa wao wa masuala
ya haki za binadamu na kuangalia kwa makini masharti yake na hata
aina ya jamii, ambamo haki hizi zinaweza kutekelezeka kwa uthabiti
zaidi. Neno “demokrasia” lilijitokeza mara nyingi, likiwa limesikika
kutoka kwenye mjadala wa kisiasa wa kitaifa, lakini hakukuwa na mtu
aliyekuwa na uhakika wa maana ya neno hilo. Hivyo wafanyakzi waliamua
kufanya majaribio ya utaratibu wa mafunzo uliohusisha dhana ya demokrasia
na mfumo wa kijamii uliopo ambamo haki za binadamu zinaweza kutekelezwa
kwa ufanisi na watu wa aina zote wanaweza kushiriki kuamua majaliwa
yao. Maudhui ya mafunzo yaliyotokana na majaribio haya yaliyodumu
kwa miezi kadha yalijumuisha taarifa (habari), majadiliano, uigizaji
na shughuli zenye matumizi yenye manufaa – vyote vikisisitiza juu
ya haki za binadamu ambazo jamii lazima izilinde, jinsi maadili binafsi
na ya vikundi yanavyowekwa sawa, kwa njia gani wale walionyang’anywa
haki zao wanaweza kuzidai, jinsi gani mizozo hutatuliwa, na mikakati
ya uongozi bora inayohitajika kwa ajili ya malengo ya aina hii. Waandaaji
waliona ni vema kurejea maana ya msingi ya “demokrasia” katika Kigiriki
– yaani serikali inayoendeshwa na watu – na kutoa nafasi kwa majadiliano
mapana juu ya kilichomaanishwa hasa na dhana hii na jinsi ilivyohusishwa
na madai ya haki za binadamu na utatuzi wa mizozo. Demokrasia ilifasiliwa
na kujadiliwa kama mpango unaoathiri maisha ya familia na jumuiya
za vijiji kama unavyoathiri pia siasa katika ngazi ya mkoa au taifa.
Mjadala na mabadilishano ya mawazo juu ya mada hizi katika jumuiya
zilizoshiriki ulikuwa wa kusisimua na punde ukavuka mipaka ya kozi
ya elimu isiyo rasmi. Mazungumzo mengi ya pande mbili kati ya wanaume
na wanawake, vijana na wazee, na hata baina ya kabila mbalimbali yalijitokeza
katika maeneo mengi yaliyohusishwa kwenye mradi huu. Kutunza imani ya wananchi Waandaaji
walijali sana kushirikisha mamlaka za vijiji na viongozi wa kidini
katika programu hii. Kusema kweli, pengine kichocheo kikuu cha mpango
huu ulikuwa mwingiliano na maadili ya kidini, hasa ile ya Kiislamu,
katika maeneo husika. Mtazamo wa waumini wengi ulikuwa kwamba haki
na kanuni za kidemokrasia zilizokuwa zikijadiliwa ziliakisi vema zaidi
maadili ya Kiislamu kuliko ya jamii ya kisasa au desturi za kileo. Matokeo
ya dhahiri yalionekana punde katika nyanja mbalimbali. Msukumo mkubwa
ulielekea kutokana na falsafa ya Gandhi ya kutotumia nguvu – yaani,
kutokana na juhudi za makusudi za kuwafanya wananchi kutambua ukinzani
kati ya maadili na mienendo halisi. Ukatili dhidi ya wanawake na watoto
katika familia unatoa mfano hai. Washiriki wa programu ya elimu ya
demokrasia ya Tostan walishutumu tabia ya kuwapiga wake na watoto
katika familia. Matukio halisi ya vipigo yalitolewa na kujadiliwa
katika jumuiya mbalimbali. Kama kiongozi wa kiume wa kaya katika kijiji
cha Ngaparou alivyosema “sote tulijua kwamba haikuwa haki kuwapiga
wanawake. Tulifanya hivyo kwa mabavu tu. Lakini hatuna budi sasa kubadilika,
kwa sababu jambo hili sasa linachukuliwa kuwa ni uovu na watu wote.
Ni jambo lililo hadharani. “Kuwa hadharani” – ingawa kwa kawaida si
kwa namna ya ushari – ndiyo imekuwa zana kuu ya mabadiliko haya”. Haki
za watoto ni jambo jingine muhimu linalotiliwa mkazo. Vikundi vingi
katika mji wa Thies vilivyoshiriki kwenye programu hii vilibaini kuwa
kukosekana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wengi katika jumuiya
zao ilikuwa mojawapo ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Jambo
hili lilipaswa kurekebishwa, kwani liliwazuia watoto hawa kujiandikisha
shuleni na kupata fursa nyingine za maisha bora. Washiriki wa programu
walishawishi uanzishwaji wa taratibu mpya na upatikanaji na vyeti
vya kuzaliwa kwa idadi kubwa ya vijana. Katika baadhi ya maeneo ya
mkoa, tatizo la ndoa za utotoni bila ridhaa ya wasichana lilijadiliwa
pia kwa kina. Ongezeko la msisitizo juu ya haki za wasichana lilipelekea
pia kwenye upigwaji marufuku tabia ya kutahiri wanawake – jambo lililojadiliwa
kwenye IK Notes # 3 kuhusu Kiapo cha Malicounda. Desturi za uwajibikaji Mjadala
wa demokrasia unaelekea pia kuwa na athari kubwa kwa utendaji kazi
wa vyama vya kijumuiya na jumuiya zenyewe. Dhana za uwajibikaji, uwazi,
sifa za uongozi, uwakilishi wa vikundi mbalimbali na utawala bora
zilijadiliwa sana kwenye mtaala kama ilivyokuwa pia kuhusiana na mbinu
za kutatua mizozo inayoletwa na madai ya kutambulika kijamii na ya
usawa. Wafanyakazi wa Tostan wanawaona washiriki wa awali wa programu
hii wakikiri kuwa pamekuwepo na mabadiliko makubwa katika taratibu
na hata watumishi wa vyama vya kijumuiya kutokana na mafunzo haya.
“Sasa tunajua vizuri zaidi sifa za kiongozi”, wanasema: na kuna ongezeko
kubwa la ushiriki wa wanawake katika shughuli za uongozi. Aidha wanawake
hawataki tena kuvumilia utaratibu wa kijadi ambapo kiongozi – wa kiume
au wa kike – hutoa maamuzi kwa ajili ya washirika wenzake. Na katika
maeneo kadhaa vituo vya kutatua mizozo vimeanzishwa na wanawake waliohitimu
mafunzo ya demokrasia. Zaidi
ya hayo, yapo pia madai mengine ya kisiasa. Washiriki wanadhani kuwa
idadi kubwa zaidi ya wanawake wanapendelea kupiga kura kuliko ilivyokuwa
hapo awali – na wachache wanaukubali utaratibu uliozoeleka ambapo
kiongozi wa kiume wa kaya huwaelekeza wanafamilia wote jinsi ya kupiga
kura. (Kwa hakika katika baadhi ya vijiji chifu ndiye aliyeamwua namna
wakazi wake wote watakavyopiga kura). Mjadala juu ya sifa za kiongozi
umepelekea kuanzishwa kwa vigezo vipya vya kuwatathimini wagombea
wa nafasi za uongozi wa kisiasa katika baadhi ya maeneo. Orodha mahususi
ya vigezo hivyo ilitayarishwa na wagombea wakahitajika kuwa na idadi
kubwa ya vigezo hivyo kabla ya kuteuliwa kushika madaraka. Wanawake
wa eneo la Fouta Toro waliazimia kufuatilia kwa karibu utungaji wa
sheria za kitaifa ili uzingatie haki za binadamu. Sekta inayokua Dai
la mafunzo ya demokrasia limekuwa likiongezeka na kuchochea ari ya
kupigia kampeni masuala ya haki za wanawake. Washiriki kutoka visiwa
vya Sine Saloum kiangazi hiki walitumia mitumbwi kuzifikia jumuiya
mbalimbali katika eneo lao ili kuunda umoja dhidi ya tohara za wanawake.
Zaidi ya vijiji themanini, vilivyoenea takribani katika tarafa nzima
ya Dabo, vimejiunga na umoja huu kwa hiari yao. Na katika maeneo ya
Toucouleur ya Fouta Toro washiriki wa programu ya mafunzo wameanzisha
“maonyesho ya barabarani” ambayo huonyeshwa kwenye vijiji mbalimbali
vya maeneo hayo. Matokeo
yameonekana pia kwenye maeneo ya mbali kabisa. Washiriki kutoka eneo
la Ngirin Bamba walianzisha mradi wa bustani kwa kuomba mashamba kutoka
kwa wanaume wa kijijini kwa msingi wa “ardhi kwa mkulima” – na kisha
wakaweka bango kwenye lango la bustani yao ya mboga za majani na matunda
lililosomeka “haki ya kumiliki ardhi”. Hivyo
dhana za “demokrasia” – zinazozingatia mazingira halisi ya Senegal
zinajumuishwa katika madai haya mbalimbali ya haki za binadamu. Neno
lenyewe limekopwa moja kwa moja katika lugha za Kiwolof na Kifulani/Kipulaar
na kutumika mara kwa mara katika mabishano, matangazo, na utani kwenye
vijiji vyote vinavyoshiriki katika programu ya mafunzo. Kama mwanamke
mmoja wa Ker Simbara alivyomweleza mwendesha mafunzo aliyetembelea
huko kufuatilia utekelezaji wa programu, “tulilazimika kubadilisha
uendeshaji wa mikutano yetu ya ushirika kwa sababu tulibaini kuwa
ilikuwa haiendani na “demokrasia”. Wakati majaliwa ya serikali ya
uwakilishi wa kitaifa yangali mashakani katika bara lote la Afrika,
iaelekea demmokrasia inayozingatia mazingira halisi ya eneo husika
ndiyo itakayopendelewa na nchi nyingi siku za usoni. *Msingi wa makala hii ni utafiti uliofanywa na watafiti wa Senegal kwa msaada na ushauri wa kiufundi wa Profesa Peter Eastom wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Florida, wakishirikiana na baadhi ya jumuiya za Kiafrika. Utafiti ulifadhiliwa na Club du Sahel OECD, CILSS na ADEA. |