THE WORLD BANK GROUP A World Free of Poverty
Home


Kwanini

Kwanini ni muhimu

Malengo

Mafanikio

Kiunzi cha utendaji

MA kwa mtazamo wa Haraka

Databesi

Washiriki wenzi

Nini kipya

Taarifa za MA

Rasilimali za MA

Mabunda ya MA

Mrejesho

Ujuzi ni muhimu – kuelewa namna watu na jumuiya wanapata na wanatumia maarifa ni lazima kwa kuongoza maisha ya watu, hasa maisha ya mafukara. Ripoti ya Maendeleo Duniani 1998

Maarifa

Asili

kwa Maendeleo

Wanawake nchini Mali wanoatia rangi kitambaani, wanatumia marembo na usanifu wa kiasili Utoaji ulioongzwa na Benki ya Dunia kushirikiana na

CIRAN/Nuffic, CISDA, ECA, IDRC, ITU,

SANGONet, UNDP, UNESCO, WHO, WIPO

Ruya za ushirikiano wa maarifa duniani hazitahakikishwa mpaka mafukara wanashirikiana hata kama wanaotumia na wanaochangia ujuzi

Majitihadi yana malengo na mafanikio gani?

Kueneza maarifa

*Tunaendelea kutengeneza databesi ya mifumo na mafunzo yaliyofundishwa na maarifa ya asili (MA)

*Tunachapisha kesi kwa karatasi na kwa kompyuta

Kurahisisha ushirikiano wa maarifa baina ya jumuiya zinazoendelea

*Tunasaidia ujenzi kijijini wa kushiriki maarifa ya asili       

*Tunatambulisha mifumo inayofaa ya kukusanya na kueneza maarifa ya asili vijijini      

*Tunarahisisha kuunganisha watu duniani kubadiliana maarifa ya asili

*Kutumia Maarifa ya Asili kwenye mfumo wa maendeleo   

*Tunaelemisha washirika wa maendeleo kuhusu umuhimu wa maarifa ya asili       

*Tunaongoza utumizi wa maarifa ya asili kwenye miradi na programu za Benki ya Dunia na washirika wake wa maendeleo

*Kutengeneza usharikiano      

*Tunajifunza kutoka kwa jumuiya za kimwetu na mashirika yasiyo ya kiserikali       

*Tunaunganisha viingiziamali vya haba vya washirika wetu kwa ajili ya kuongeza matokeo kazini     

*Tunajadiliana kuhusu mambo ya haki za uvumbuzi wa maarifa ya asili

Picha ya kijadala ilipigwa na R. Kiessling, GTZ, Eschborn

 Mfano kutoka databesi ya Maarifa ya Asili

Matumizi: Kusihia mfumo wa kilimo wa Washambaa kwenda nchi ya Rwanda, kuendekeza na kusihia tena

Washambaa wa milima Usambara, nchini Tanzania, tangu zamani wameiga mimea ya mazingira wakati wa kulima ardhi zao.  Wakulima huhifadhi rutuba wakichanganya miti na vijiti pamoja na mazao shambani.  Mfumo fani huu ulichunguzwa na mradi wa shirika la uhisani wakauleta Rwanda.  Wakulima na wafanyakazi wa maendeleo huko Rwanda waliendekeza mtindo huu na wakauongeza wakaingiza ufugaji wa ng’ombe na ulimaji wa malisho yao.  Wakulima wa Rwanda walisaidiwa kulima chakula kingi zaidi na kuongeza mapato papo hapo kutunza rutuba ya ardhi.

Mafunzo: Kuiga mimea ya mazingira ni njia sahihi ya kuhifadhi ardhi; Wakiusahia, wakiutumia, na wakiuendekeza mfumo wa asili, wakulima wanaweza kuongeza upataji wao.

Namna ya kuchangia databesi: 

Ukijua kuhusu mfumo wa asili uliofanikiwa, tunaomba ututaarifie!

Tunaomba utuambie maarifa haya:  Mfumo unatokea wapi (nchi na mahali)?  Kutoka kwa nani (k.m., Washambaa, waganga wa kienyeji)?  Katika sehemuduara gani (kilimo, afya)?  Kutumia teknolojia gani (k.m. kuhifadhi ardhi isizorote, kulea watoto).  

Tunaomba ueleze vipengee vikuu vya mfumo huu, na kwa nini ni muhimu kijijini?  Kwa nini ni muhimu miradi ya maendeleo ijifunze zaidi kuhusu mfumo huu?  Utafaidiaje jumuiya nyingine?  Na tukitaka kuelewa zaidi, tuulize wapi: usisahau jina lako, anwani, simu, faksi, na, ikipatikana, email yako.

Ni muhimu kwa nini?

Maarifa ya asili yanaauni mikakati ya kutatanua mashida kwa jumuiya za wenyeji, hasa watu maskini.  Yanachangia michango muhimu kwa maarifa ya maendeleo duniani.

Maarifa ya asili hayatumiwa ya kutosha kwenye mfumo wa maendeleo.

Kwa nini ni muhimu jumuiya ya maendeleo tujali?

Tukijifunza kutoka kwa maarifa ya asili tunaweza kufahamu zaidi hali halisi kimwetu.

Tukifahamu maarifa ya asili tunaweza kuwaitikia wateja wetu.

Tukiendekeza mifumo ya kimataifa kuzingatia hali halisi kijijini tunaweza kuboresha matokeo na uendelevu wa kazi yetu.

Gharama zinazotumiwa kueneza maarifa ya asili zinaweza kupunguza umaskini. 

Kushirikiana Maarifa ya Asili ndani ya na baina ya jumuiya kunaweza kuongeza uelewano wa watu duniani.

Uanzishaji wa majitihadi

Mkutano wa Ujuzi Duniani, uliotokea mjini Toronto mwezi sita mwaka 1997, ulitamka mahitaji muhimu ya kujifunza, kutunza, na kubadilishana maarifa ya asili.  Ndani ya Shirika la Teknolojia za Kutangaza na Kuwasiliana kwa Afrika (PICTA), Benki ya Dunia imekubali kuongonza Majitihadi ya Maarifa ya Asili kumotisha utambuzi, utumizi, na ubadili wa maarifa ya asili kwenye mfumo wa maendeleo.

Maarifa ya asili ni nini?

Maarifa ya asili ni ya pekee kwa kila utamaduni na jumuiya.  Ni msingi wa uamuzi wa kimwetu katika kilimo, afya, hifadhi ya mazingira, na utenzi wengine.  Maarifa ya asili yanakaa ndani ya mifumo, madhehebu, mahusiano, mila na desturi za jumuiya.  Maarifa ya asili yanahusika maisha ya kila siku, kama madawa ya kienyeji, uganga wa kienyeji wa sindano, na kadhalika.

Washirika ni nani?

CIRAN/Nuffic, CISDA, ECA, IDRC, ITU, SANGONet,

Benki ya Dunia (Mshirika Kuu), UNDP, UNESCO, WHO,

WIPO

Muungano Duniani wa MA, taasisi za maarifa ya asili katika nchi zinazoendelea.

Tunatafuta washirika wengine…

Namna ya kuwasiliana nasi:

Tunakaribisha michango, fikra, na masuali.

The World Bank/ Benki ya Dunia
Africa Region Knowledge and Learning Center
Reinhard Woytek
1818 H Street NW
Washington, DC 20433 USA
Tel.: +1 202 473 1641
Fax: +1 202 477 2977
E-mail: rwoytek@worldbank.org
Website at URL http://www.worldbank.org/afr/ik

 


Footer